Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kama Unataka Kuandika Historia Ya Maisha Yako

Kila mtu anao uwezo mkubwa wa kuandika historia ya maisha yake, lakini utaandikaje historia ya maisha yako kwa namna unavyoishi maisha ambayo siyo yako?

Asilimia kubwa ya maisha wanayoishi watu siyo maisha yao halisi, wengi wanaigiza kuonekana wana maisha fulani lakini usiku wakiwa peke yao nafsi zao huwa zinawasuta, utawadanganya watu wote lakini huwezi kuidanganya nafsi yako hata siku moja.

Je hayo ndiyo maisha yako halisi? Huwezi kuandika historia ya maisha yako kama unaishi maisha ya kuigiza ambayo siyo halisi.

Ukitaka kuandika historia ya maisha yako anza kuishi leo maisha yako na hapo ndiyo utaweza kufanya makubwa na kuweza kuandika historia nzuri. Unapaswa kujiuliza je maisha ninayoishi yanajenga historia gani? Je historia ninayojenga itasomekaje mbele ya watu? Ni nzuri au mbaya? Wewe ndiyo unajua kama unayofanya yanajenga historia nzuri au mbaya.

Usiwe wakala wa kuandika historia mbaya kwenye maisha yako. Kuwa wakala wa kuandika historia nzuri ya maisha yako ambayo itaweza kuja kusomwa hata na vizazi vijavyo. Dunia inakusubiria ufanye mambo makubwa ili nayo ifaidi kutoka kwako na siyo kuishi maisha ambayo siyo yako.

Hatua ya kuchukua leo; Nenda ukaishi maisha yako vizuri ili uandike historia nzuri ya maisha yako. Huwezi kuandika historia ya maisha yako kama hujawahi kuishi maisha yako.
Kuwa wewe, na ishi kama wewe usipoteze muda wa kuigizia watu jua unajidanganya na kujichelewesha na unatakiwa kujua unaishi mara moja tu hivyo ukishindwa kuishi leo jua umekubali kupoteza maisha yako.

Kwahiyo, historia ya maisha yako inajengwa na wewe mwenyewe lakini haijengwi kwa kuweka mikono mifukoni na kujadili mambo ya watu bali kwa kuweka kazi. Badilisha historia ya maisha yako kwa kwenda kufanya kazi na siyo maneno.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz  

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

2 Comments

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: