Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndiyo Kitu Cha Maana Zaidi

Natumaini una ndoto, je, ndoto yako imefikia wapi? Iko kichwani au iko kwenye matendo?

Huenda una ndoto na hujui namna ya kufikia ndoto yako, kama una ndoto na hujui namna ya kufikia ndoto yako, jipatie nakala ya kitabu kinachoitwa jinsi ya kufikia ndoto zako kwa mifano kilichoandikwa na Godius Rweyongeza. Kitakusaidia kupata mwongozo kwenye safari yako.

Steve Jobs aliwahi kunukuliwa akisema, kuwa tajiri kaburini siyo kitu ambacho ningependelea… Ila kwenda kulala usiku huku nikisema kwamba nimefanya kitu cha maana ndiyo jambo la maana zaidi.

Makaburini kuna utajiri mwingi kwa sababu wako watu wengi walikufa na ndoto zao na hivyo kuzikwa nazo. Fanyia kazi ndoto yako kuna watu wanaisubiria ili wao nao waweze kutimiza ndoto zao.

Aliyetengeneza smart phone kwa mara ya kwanza Steve Jobs amesaidia kutimiza ndoto za watu wengi. Hebu tu fikiria katika zama zetu maisha bila smart phone au simu janja yangekuwaje? Ni wangapi wametimiza ndoto zao kwa kuwa tu na smart phone?

Usikubali kwenda na ndoto yako kaburini bora uanze kuifanya kazi leo.

Unapokwenda kulala usiku, jiulize umefanya kitu cha maana katika kutimiza ndoto yako? Kama jibu lako ni ndiyo basi utakua umefanya kitu cha maana zaidi.

Jambo la maana zaidi ni kufanya kitu katika siku yako. Usikubali siku ipite bila kufanya kitu cha maana.

Ukichukua hatua unakua umefanya jambo la maana. Usipochukua hatua umekubali kupeleka utajiri wako makaburini. Kubali kuruhusu utajiri wako kutumika ukiwa hai na siyo kwenda kuuzika makaburini.

Waliolala makaburini, wengi wamelala na ndoto zao ambazo walipaswa kuzitimiza.

Kuwa mtu tajiri kaburini siyo kitu ambacho unapendelea hivyo usikubali itokee hivyo anza kuwa mtu tajiri ukiwa hai na siyo kusubiria kufa na ndoto yako.

Hatua ya kuchukua leo; Jiambie, nitatimiza ndoto yangu kwa kuchukua hatua sahihi kila siku.

Kuchukua sahihi leo ni jambo la maana zaidi katika siku yako. Usikubali siku ipite bila kufanya kitu kwenye ndoto yako.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: