Design a site like this with WordPress.com
Get started

Siku Ya Kuchunguza Ubize Wako

Ubize ni neno ambalo linaongelewa karibu na kila mtu. Ukikutana na mtu utamsikia akisema niko bize aisee. Je, umeshawahi kukaa chini na kuhoji ubize wako? Kila siku uko bize, lini utakua huru? Je, ubize wako ni ubize hasi au chanya? Wengi wako bize je, huo ubize wao matokeo yake yanaonekana? Au ubize jina tu? Ubize …

Kitu Cha Uhakika Kupata Pale Unapothubutu Kufanya Jambo Lolote Lile

Ni changamoto. Niambie ni jambo gani ambalo utasema ulianze halafu usikutane na changamoto njiani? Kila kitu kina changamoto ndiyo maana huwa nashangaa mtu anayeacha kufanya jambo lake kwa sababu ya changamoto. Ukiingia kwenye biashara kuna changamoto zake na changamoto ni kitu cha uhakika kuliko hata faida. Ukiwa kwenye ajira nako pia kuna changamoto zake. Kifupi …

Usichague Kitu Hiki Kwenye Maisha Yako

Usichague kuwa mtu asiyekuwa na thamani. Kuwa mtu wa thamani au kutokuwa mtu wa thamani ni kuchagua. Usichague kuishi maisha ya juu ya kipato chako. Haijalishi una kipato kikubwa au kidogo unatakiwa kuishi chini ya kipato chako. Usichague kuishi bila kuweka akiba. Weka akiba mara nyingi uwezavyo kwani akiba itakuja kukusaidia hapo baadaye na uzuri …

Namna Bora Ya Kurudisha Neno Ulilozungumza

Unapozungumza unapaswa kuwa makini kwa sababu neno unaloongea ni kama vile unarusha jiwe gizani na hujui nani litampata. Ukishaongea, umeaongea na watu watatafsiri vile wanavyojua wao kadiri ya hisia walizokuwa nazo. Kifupi, namna bora ya kurudisha neno ulilozungumza ni kutolisema tu. Kuwa mwangalifu na maneno yako, kumbuka hakuna namna nyingine ya kulirudisha neno ulilozungumza isipokuwa …

Njia Nzuri Ya Watu Kujua Unauza Nini

Huwa ninashangaa sana pale ambapo mtu anakuwa anamiliki kitu kizuri ambacho ametumia gharama kukitengeneza lakini cha ajabu hana hata mpango wa masoko au mauzo. Unapozalisha kitu ili watu wengine wakipate andaa mpango wa masoko. Unaweza ukawa na bidhaa bora lakini kama watu hawaijui ni sawa na bure. Bidhaa ikishazalishwa ipeleke sokoni. Na wale ambao ni …

Hiki Ndicho Alichowahi Kusema Mwanafalsafa Antisthenes Juu Ya Adui Yako

Antisthenes ni mwanafalsafa wa kigiriki. Mwanafalsafa huyu aliwahi kusema hivi juu ya adui yako. ” Wasikilize maadui wako, kwa sababu ni wa kwanza kugundua makosa yako.” Ni kweli maadui wako huwa wanagundua makosa yako sana kuliko watu wengine. Hivyo fuata ushauri uliopata leo kutoka kwa mwanafalsafa Antisthenes. Hivi hujawahi kujiuliza ni kwa nini Yesu alisema …

Tumia Njia Hii Kujihamasisha Kufanya Makubwa Kwenye Maisha Yako

Njia yenyewe ni kifo. Ukifikiria majukumu uliyonayo, watu wanaokutegemea katika familia yako huku ukifikiria siku yoyote utakufa huwezi kufanya ujinga utajisukuma kufanya makubwa. Aliyekuwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Magufuli kila mara katika hotuba zake alikuwa anaongelea kifo. Anasema kama akifikiria siku moja atakufa je akifa leo hii miradi aliyoiacha nani …

Hii Ndiyo Mitego Unayopaswa Kuitega Kama Unataka Kufanikiwa Zaidi

Kama unataka kupata fedha zaidi inakupasa utoe thamani zaidi. Fedha haziwezi kuja tu kwako kama huna mitego ya kuinasa. Mitego mizuri ya kunasa fedha ni kuwa na vitega uchumi vingi. Yaani unakuwa unatoa thamani kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato ulivyotega. Tabia mojawapo ya fedha inapenda mtu mbunifu. Usipokuwa mbunifu wa miradi mbalimbali fedha zitakukimbia na …

Maswali Mawili Ya Kujiuliza Kila Siku Asubuhi Na Jioni

Hakuna anayeamka asubuhi na kupanga kuwa na siku ya hovyo. Kila mmoja wetu anapenda kuwa na siku bora na ndiyo lengo la kila m Ili uweze kuimiliki siku yako lazima uweke mipango ya kumiliki siku yako. Usipojiandaa kuimiliki siku utakuja kumilikiwa. Usipojiandaa kutawala, utatawaliwa. Usipojiandaa kushinda, utashindwa. Jiandae kupata kile unachotaka na siyo vinginevyo. Hapa …