Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ukitaka Kujua Mtu Ni Msafi Mwangalie Sehemu Hii

Mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema kuwa, ukitaka kujua kama mtu ni msafi basi mwangalie kucha zake. Hebu ziangalie kucha zako zikoje?Chafu au safi? Kucha huwa zinabeba uchafu mwingi. Unaweza kuwa msafi wa mwili, mavazi lakini kucha zako ni chafu. Kucha zikiwa ndefu huwa zinakusanya uchafu. Ni rahisi kujiona wewe ni msafi na wengine ni wachafu kama …

Huyu Ndiye Mwenye Haki Ya Kukosoa

Kila mtu anapenda kukosoa. Na wale ambao hawana wanachofanya ndiyo kazi yao. Watu wengi wanaokusema juu yako hawajawahi kutembea katika viatu vyako. Watu watakusema kwa chochote, kwa lolote lile. Uwe umefanya mazuri au mabaya. Asiyesemwa ni yule ambaye hafanyi lolote, asemi lolote. Hata maiti inasemwa licha ya kuwa imekufa. Wewe usikwepe kusemwa, fanya kazi yako. …

Zawadi Nzuri Ya Kumpa Adui Yako

Ni msamaha.Wasawahili wanasema, adui yako akaangukapo mnyanyue. Ni hasara sana kuwachukia maadui zako kwa sababu unawapa uwezo wa kukutawala wewe. Badala ya kufanya yako, unakuwa unatumia muda mwingi kumfikiria adui. Kusamehe ni kwa faida yako mwenyewe wala siyo kwa ajili ya adui yako. Chuki ni kama kunywa sumu ukitumaini kuwa itawaua adui zako. Aliwahi kusema …

Hii Ndiyo Sababu Inayokufanya Uyaone Maisha ni Magumu

Matatizo uliyokuwa nayo tayari yanakutosha hivyo huna haja ya kuhangaika na matatizo mengine wakati hayo uliyonayo tayari yanakutosha. Kwanini unaona maisha ni magumu? Kwa sababu unajisumbua sana na mambo ambayo hayajatokea. Ukweli ni kwamba watu wanahangaika sana na mambo ambayo hayajatokea. Wanashindwa kuishi sasa na kufanya kile kinachowapasa kufanya sasa. Wakati muhimu wa kufanya maisha …

Hapa Ndipo Mahali Furaha Ilipofichwa

Nilipokuwa nasoma kitabu cha Matatizo si Tatizo kilichoandikwa na mwandishi Fr Dr Faustine Kamugisha nilikutana na hadithi moja ya mahali furaha Ilipofichwa. “Mungu alitaka kuficha furaha. Alijiambia nikiificha nchi za kigeni watu watafika huko. Nikiificha kwenye mamlaka watu watatafuta mamlaka mpaka wayapate. Nikiificha kwenye uzuri, watu watajipodoa, nikiificha kwenye biashara watu watafanya biashara waipate. Nikiificha …

Haya Ndiyo Matokeo Ambayo Huwezi Kukwepa

Hakuna eneo ambalo watu wengi wanakwama kama eneo la uchaguzi.Uchaguzi ni mtihani ambao kila mmoja wetu anapaswa kuujibu. Ukitaka kuoa au kuolewa lazima utafanya uchaguzi. Ukitaka kununua nguo lazima utafanya uchaguzi ni nguo gani ununue na ipi usinunue.Ukitaka kununua gari lazima utafanya uchaguzi ni aina gani la gari utanunua. Karibu kila kitu ambacho unacho sasa …

Njia Rahisi Ya Kuwa Tajiri

Ni kurithi. Kama hauko kwenye njia hii ya kurithi basi pambana ili uweze kupata kile unachotaka. Kama hauko kwenye kurithi basi unapaswa ujiambie kuwa, utapambana kupata kile unachotaka au utakufa huku ukiwa unapambana kupata kile unachotaka. Kila mtu amezaliwa hana kitu. Lakini, baada ya kukua watu wanaweka juhudi na kisha wanafanikiwa kwenye kile wanachotaka. Maisha …

Amua Kuacha Kitu Hiki Kwenye Maisha Yako

Mwanasayansi Albert Eistein aliwahi kunukuliwa akisema, ujinga ni kufanya kitu kile kile kwa mtindo ule ule halafu huku ukitegemea kupata matokeo tofauti. Kabla ya kwenda mbali jitathimini je unafanya ujinga? Yaani kila siku, kila mwezi, kila mwaka huna unachofanya cha tofauti zaidi ya kufanya kitu kile kile kwa mtindo ule ule. Halafu unajiambia utafanikiwa siku …

Usiwe Kama Bahari Hii Hapa

Kuna bahari moja iko katika nchi ya Israeli. Inayojulikana kama bahari mfu yaani Dead Sea. Sifa moja ya hii bahari ni kupokea maji halafu haitoi. Matokeo yake maji yake hayafai kwa matumizi ya binadamu. Hii ni bahari ya ajabu, inapokea tu bila kutoa. Na cha ajabu ni kwamba nayo kama vile imelaaniwa ina maji lakini …

Hiki Ndiyo Chanzo Cha Matatizo Yako Yote

Waswahili wanasema, liwezekanalo leo lisingoje kesho. Kuna mtu mmoja alisema, “kusitasita ni chanzo cha matatizo yangu yote. Hata hivyo sijui maana ya neno kusitasita kesho nitatazama maana yake kwenye kamusi” Hapa tunaona ni jinsi gani mtu huyu alikuwa bado na tatizo la kusitasita. Maadui wa kutumia fursa za leo ni kusitasita na kuahirisha mambo. Hebu …