Jinsi Ya Kujua Kama Unajua

Kila mtu anajua na kila mmoja wetu amezaliwa na tabia za kijiniazi. Changamoto ya watu wengi ni kushindwa kutumia vizuri rasilimali walizopewa na Mungu.  Wengi kinachowamaliza ni ile hali ya kuridhika, kutopenda kujisumbua kwa ajili ya wengine. Hii niliyokuwa nayo inatosha, hii kauli ya ubinafsi, hatupendi kujisumbua kwa ajili yetu wenyewe na hata wengine. Tunapenda …

Ukitaka Kumjua Mtu Alivyo Mpe Vitu Hivi Viwili

Tabia huwa hazidanganyi zinasema ukweli. Je ulikuwa unajua kwamba asilimia 40 ya matendo yanayofanyika kila siku siyo maamuzi bali ni tabia. Kile wanachofanya watu wengi kila siku ni tabia zao na wala siyo maamuzi. Binadamu anachofanya ni tabia sana kuliko maamuzi anayofanya. Mtu ni tabia, hivyo katika maisha jifunze sana kupitia tabia za watu kuliko …

Hiki Ndiyo Kitakachoweza Kukutoa Hapo Ulipo

Kila mtu anapenda kutoka katika maisha yake. Tunapenda mafanikio kwenye maisha yetu lakini mafanikio haya tunayoyataka yanaletwa na kitu kimoja ambacho mtu akikubaliana nacho ataweza kufanikwa sana. Matendo yetu huwa hayaendani na kile tunachokipenda kwenye maisha yetu. Hatuweki juhudi za kweli zinazoendana na kile tunachotaka hasa. Tunaishia tu kuongea kwa mdomo. Kama unataka kufanikiwa jiambie …

Jaribu Kufanya Kitu Hiki Ili Upate Faida Hii Muhimu Kwenye Maisha Yako

Kujaribu siyo kushindwa ,je unajaribu mara ngapi kufanya vile unavyotaka kufanya ili ufanikiwe kwenye maisha yako? Mara nyingi huwa tunajaribu na kushindwa, wengine wanajaribu na kushinda sasa inapotokea pale mtu anajaribu akashindwa ndiyo unakuta anakata tamaa kabisa kwenye maisha yake. Madalyn Murray O’Hiar aliwahi kusema; sijali kama nafanikiwa au nashindwa ilimradi najaribu. Natumaini nitafanikiwa. Hiyo …

Jinsi Unavyopoteza Kiasi Kikubwa Cha Fedha

Kama kila mtu angekuwa anajiwekea fedha katika akaunti maalumu ya uwekezaji basi leo kila mtu angekuwa vizuri sana kifedha. Tunapoteza kiasi kikubwa cha fedha pale tunapokuwa tunatumia fedha zote tunazozipata bila kuweka akiba. Kwa mfano, ungekuwa unaweka akiba yako kwa miaka mitano iliyopita leo hii ungekuwa mbali sana. Nakushauri fungua akaunti ya uwekezaji katika mfuko …

Huwezi Kushinda Siku Zote Ila Unaweza Kujifunza Siku Zote

Licha ya kujiandaa na ushindi lakini siyo kila wakati mambo yanaweza kwenda kama vile tunavyotaka sisi. Tunapokuwa tunapanga mambo yetu na dunia inapanga. Hatuwezi kuizuia dunia kufanya vile inavyotaka bali tunatakiwa kukubaliana na asili ya dunia. Hatuwezi kushinda kila wakati, kuna muda tunashindwa hivyo ni jambo la kawaida hilo kila mtu anaalikwa kulifahamu hilo. Hatujui …

Hiki Ndiyo Kitu Pekee Ambacho Hakiwezi Kukufikisha Kwenye Mafanikio

Heri ya mwezi April, Ni kawaida watu kuishi bila mipango au malengo, hata ukiwauliza watu nini malengo yako ya mwezi huu tulioanza leo huenda hata asikupe majibu sahihi. Tumekuwa ni wazuri sana katika kuongea kuliko utendaji wa kazi. Watu ni wazuri wa kuweka mipango lakini kwenye utekelezaji ni watu wagumu sana kufanya. Uongo wa watu …

Hii Ndiyo Zawadi Bora Unayoweza Kujipatia Mwisho Wa Mwezi Huu

Mwanamafanikio, Katika maisha kuna mambo mawili kwenda mbele na kurudi nyuma. Watu wengi wanafikiria maisha yanakusimama,hapana maisha hayasimami hata siku moja. Kama ukiona huendi mbele basi unarudi nyuma na kiyume chake ni sahihi. Hakuna mtu anayeweza kusema mimi kwa sasa nimesimama kidogo kuishi labda nitaanza mwakani tena kuishi. Maisha hayasimami, pale unaposimama kuishi ndiyo unakuwa …

Usitarajie Kupata Kitu Hiki Kwenye Maisha Yako

Kila kitu kinahitaji kazi, kazi bila kazi hiyo siyo kazi. Najua hapo ulipo kuna kitu unatarajia kukipata hivyo usitegemee kukipata kama hujakiwekea kazi. Usitarajie kupata kitu chochote kama hujakiwekea kazi. Ukitaka ufanikiwe kwenye eneo fulani la maisha lazima uliwekee kazi. Usitarajie kupata kitu bure, hata cha bure kina gharama yake.  Usidanganyike kwenye chochote kwamba utaweza …

Hii Ndiyo Lugha Bora Ya Kufundishia Watoto

Rafiki, Kila mmoja wetu alikuwa mtoto, kama unasoma hapa huenda una mtoto au unatarajia kupata mtoto. Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, hivyo tunatakiwa kujifunza namna ya kuwalea watoto hawa ambao tumepewa kama zawadi. Wazazi wengi wanajua kuzaa lakini kwenye malezi kuna ubinafsi mkubwa. Unaweza kukuta mzazi anajijali yeye lakini ukienda kumuangalia mtoto wake, hawafanani …

Design a site like this with WordPress.com
Get started