Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndiyo Kitakachoweza Kukutoa Hapo Ulipo

Kila mtu anapenda kutoka katika maisha yake. Tunapenda mafanikio kwenye maisha yetu lakini mafanikio haya tunayoyataka yanaletwa na kitu kimoja ambacho mtu akikubaliana nacho ataweza kufanikwa sana.

Matendo yetu huwa hayaendani na kile tunachokipenda kwenye maisha yetu. Hatuweki juhudi za kweli zinazoendana na kile tunachotaka hasa. Tunaishia tu kuongea kwa mdomo.

Kama unataka kufanikiwa jiambie ukweli. Ukweli huwa unauma sana na haujawahi kumwacha mtu salama hata siku moja. Ukweli haupendwi na watu wa kawaida kwa mfano, nenda kamwambie mtu masikini kwamba yeye ni masikini kwa sababu ya moja mbili tatu atakuambia unamdharau baada ya kumwambia ukweli.

Mwambie mtu afya yake ni mbovu, ana uzito mkubwa hivyo anatakiwa kufanya mazoezi atakuchukia, ataona wewe haufai unamnyanyasa na hali yake. Ukweli unaibua mengi ambayo yamelala ndani ya mtu. Ukweli ndiyo utaweza kukutoa hapo ulipo.

Sasa wengi wanapotaka kufanikiwa wanaukimbia ukweli hawataki kujiambia ukweli na kuufanya ukweli kuwa sehemu ya maisha yao. Jiambie ukweli kama ulivyo bila kupindisha, angalia sababu ambazo zinakufanya wewe ushindwe kufanikiwa nini, ziorodheshe kabisa bila kudanganya halafu anza kuzifanyia kazi moja baada ya nyingine. Bila kukubali unaumwa huwezi kujitafutia tiba sahihi.

SOMA; Hii Ndio Faida Ya Kuongea Falsafa Ya Ukweli Katika Maisha Yako

Jiambie ukweli, kama uko katika hali mbaya ya mahusiano jiambie ukweli bila kuficha. Kama uko katika hali mbaya ya kiuchumi jiambie ukweli bila kuficha. Watu wengi wako katika hali mbaya ya kifedha lakini hawataki kujiambia ukweli kwanini wako katika hali mbaya ya kifedha.

Ukijiambia ukweli wewe ni mzembe na afya yako, una matumizi mabaya kifedha itakuwa rahisi kwako kuchukua hatua kuliko kujiambia mambo siyo mabaya sana.

Hatua ya kuchukua leo; jiambie ukweli kama unaona mambo hayako sawa na baada ya kujiambia ukweli chukua hatua mara moja iwezekanavyo.

Kwahiyo, usijionee huruma kujiambia ukweli, jiambie ukweli ili ukuume na uchukue hatua. Ukitaka watu wajibadilishe waambie ukweli bila kuficha hata wakikuchukia utakua umewasaidia.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: