Rafiki,
Kila mmoja wetu alikuwa mtoto, kama unasoma hapa huenda una mtoto au unatarajia kupata mtoto.
Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, hivyo tunatakiwa kujifunza namna ya kuwalea watoto hawa ambao tumepewa kama zawadi.
Wazazi wengi wanajua kuzaa lakini kwenye malezi kuna ubinafsi mkubwa. Unaweza kukuta mzazi anajijali yeye lakini ukienda kumuangalia mtoto wake, hawafanani kabisa.
Tunaalikwa kuwapenda watoto, kuwajali na kuwapa ulinzi.
Watoto wanapitia magumu katika zama hizi za taarifa.
Wazazi wamekuwa bize kiasi kwamba wamesahau hata majukumu yao ya malezi.
Huwa sipendezwi na lugha ambayo wazazi wengi wanaitumia kuwafundishia watoto wao. Kama kila mmoja wetu angelifundishwa kwa lugha ambayo nakwenda kukushirikisha hapa basi jamii ingekuwa bora sana.
Lugha Bora ya kufundishia watoto ni lugha ya upendo. Wazazi wengi tumeshazoea kutumia lugha ya ukali kuwafundishia watoto.
Mtoto ukimfundisha kwa lugha ya upendo ni rahisi kuelewa na kukumbuka kuliko lugha ya ukali.
Lugha ya ukali inajenga hofu kwa watoto.
Lugha ya ukali inaharibu ubunifu na kipaji cha mtoto wako.
Ukitaka mtoto wako umfundishe na awe mwelewa na akukumbuke mfundishe kwa lugha ya upendo. Kila mmoja wetu anapenda upendo , hivyo kama tukifundishwa hata sisi wenyewe kwa upendo tunakua tunafurahia iweje sasa kwa watoto wetu tunakwenda kinyume?
Ni wakati wa kubadilika sasa, tutumie lugha ya upendo kuwafundishia watoto wetu badala ya lugha ya ukali.
Tuwapende watoto wetu bila kipimo. Kwani kipimo cha upendo ni kupenda bila kipimo.
Hatua ya kuchukua leo; Jenga urafiki na mtoto wako unapokuwa unamfundisha. Tumia lugha ya upendo kumfundishia mtoto wako na utaibua uwezo mkubwa wa ndani alionao mtoto wako.
Kwahiyo, hata mtoto anapokosea wakati wa kujifunza mfundishe kwa lugha ya upendo atakuelewa zaidi kuliko lugha ya ukali.
Kwenye upendo tunaibu mambo chanya ila kwenye ukali tunaibua mambo hasi.
Rafiki uwe na siku njema.
Makala hii imeandikwa na ;
Mwalimu Deogratius Kessy
Ambaye ni mwalimu, mwandishi na mjasiriamali.
Unaweza kujiunga na kundi lake la Wasapu lijulikanalo kwa jina la Mimi ni mshindi nimezaliwa kushinda kwa kutuma ujumbe kupitia namba hii 0717101505 kwa wasapu tu.
Pia, anakualika uweze kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya barua pepe kwa kujaza email yako hapo chini kwenye fomu.
Karibu sana mwanamafanikio tuendelee kuwa pamoja.
Asante sana.
http://www.mtaalamu.net/kessydeo
kessydeo@mtaalamu.net
deokessy.dk@gmail.com