Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha The 50 Cent

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa uko salama na unaendelea vizuri katika shughuli zako za kila siku.
Hongera kwa zawadi ya siku hii ya leo natumaini utakwenda kuitumia vizuri vilivyo. Nipende kuchukua nafasi hii tena kukualika katika makala yetu ya leo.

Kama ilivyokawaida yetu kila siku ya jumamosi inapompendeza Mwenyezi Mungu huwa tunashirikishana uchambuzi wa kitabu nilichokisoma. Leo kupitia kitabu cha The 50th Cent nitakwenda kukushirikisha Yale muhimu niliyojifunza.

Kitabu hiki ni kizuri sana kwani kinaelezea Maisha ya msanii 50 cent mbinu alizotumia hatimaye kufanikiwa. Hakika kwa Mara ya kwanza nilikua na shauku ya kutaka kujua nini alichoandika 50 cent na mwandishi mwenzake kupitia kitabu hiki.

Mambo 20 niliyojifunza katika kitabu cha The 50th Cent kilichoandikwa na 50 cent na Robert Greene ni kama ifuatavyo; karibu tujifunze wote kwa pamoja mpendwa msomaji.

1. Kama ukiipa hofu nafasi katika maisha yako Itakumalizia nguvu na hata mwendo kasi wako pia. Kama hofu imekutawala basi huna nguvu. Hofu amekuwa adui wa kunyonya nguvu za watu. Hivyo hutakiwi kuogopa bali unatakiwa kuishinda hofu na kuipa talaka kabisa.

2. Katika utafutaji wewe kama ndio mtafutaji lazima ujue utapitia changamoto nyingi. Haijalishi unapitia changamoto gani bali wewe kuwa na shabaha yako ya kufika pale unapotaka. Unapatwa na majaribu mengi na watu wa karibu kwako kama marafiki watakukimbia na kukuacha kama ulivyo. Unatakiwa kuishinda hofu na kuwa mtu jasiri na mwenye nguvu kubwa ya kukabiliana na changamoto. Usikate tamaa wewe pambana mpaka uwe mshindi katika maisha yako.

3. Dunia ya leo inahitaji uwe makini sana. Huwezi kujua kusudi la mtu ni nini kwako unatakiwa kuishi kwa tahadhari kubwa. Jua dunia inaendaje, fahamu unaenda wapi fahamu uhalisia wa maisha utakupa nguvu ,kujiamini na mwanga pia.

4. Vyovyote unavyokumbwa na changamoto katika maisha yako jaribu kutafuta mzizi wa tatizo. Chimba chimba kwa undani mpaka ukute mzizi au kiini cha tatizo. Raha ya tatizo ujuwe mzizi au kiini cha tatizo ndio utapata suluhisho zuri la tatizo lako. Usichukulie mambo juu juu bali jaribu kuchimba kwa undani mpaka upate kitu cha msingi au kiini au mzizi.

5. Ishi katika falsafa ya kujitegemea. Huwezi kuwa na uhuru wa kufanya mambo yako kama bado wewe ni tegemezi. Miliki vitu vyako mwenyewe. Huwezi kuwasaidia watu kama wewe mwenyewe bado ni tegemezi. Kuishi chini ya himaya ya mtu ni utumwa mwenye maamuzi, unapofanya kazi kwa wengine unakuwa katika huruma yao wanakuwa wanamiliki kazi yako,wanakumiliki pia.

6. Ulizaliwa peke yako na utakufa peke yako. Fanya kile ambacho ni sahihi kwako,na usiishi maisha kama vile watu wanavyotaka uishi. Msaada wa kwanza katika maisha yako ni wewe mwenyewe na msaada huo upo mikononi mwako. Heshimu kile ambacho unacho kitakusaidia.

7. Pata ujuzi kwenye vitabu mbalimbali, kwa watu waliofanikiwa na wenye hekima. Usisikilize kelele za watu wanasema nini wewe angalia na elekeza nguvu zako katika kile unachofanya. Kuwa kiziwi juu ya maneno ya watu nga’ang’ania kujitegemea katika yale unayoamini na hatimaye utafika.

8. Ukisema unasubiria ukamilifu hapa duniani utaendelea kusubiri mpaka siku yako ya mwisho hapa duniani. Usisubiri ukamilifu kama unataka kuwa mtu fulani anza kuwa leo. Fanya maamuzi yako na ya heshimu pia jifunze kupitia makosa yako. Wewe ndio mkurugenzi mtendaji wa maisha yako.

9. Wakati mwingine jamii inaweza isikuelewe unafanya nini. Hasi inaweza kuwa chanya. Waoneshe watu kuwa unaweza badilisha hasi na kuwa chanya. Usisubiri mpaka kesho anza leo. Watu wote wanaoleta mabadiliko duniani ni wale ambao hawasubiri kupewa ruhusa ni wale ambao wanathubutu kwa vitendo.

10. Mambo hayawi kama unavyodhania. Huwezi kuibadilisha dunia na kutaka mambo yaende kama unavyotaka wewe. Mabadiliko yapo na lazima yatokee na changamoto zipo haziwezi kuisha zipo kwa ajili ya kutufanya sisi tuwe imara ,jasiri na kupata fursa ndani yake. Usiogope matatizo bali furahia kuyakabili na kupata suluhu.

11. Maisha yanahusisha mapambano na mapigano. Huwezi kupata kitu bila kupambana. Hata zamani katika historia zile himaya (kingdom) Imara zinazopambana mapigano na kushinda ndizo zilikuwa zinatawala. Hakuna kingdom inayochukua himaya fulani bila kupambana. Hivyo ili uweze kushinda lazima uingie uwanjani ili upambane na hatimaye ushinde. Dunia inahitaji ubabe ili uweze kushinda hata nchi zenye nguvu duniani yaani big powers hazikuwa tu big powers bali zilipambana kuweza kufika kileleni. Kama unataka upande ufike juu ya kilele cha mlima unatakiwa uanze kupanda mlima huku ukiangalia mbele na siyo na uwe umetoa mikono mifukoni.

12. Kuwa kiongozi inahitaji uwe mtu unafanya machaguo magumu. Kiongozi unatakiwa kuwa na malengo,Mtu wa mfano,mwenye maono ya mbali. Uwe mtu unayeunganisha watu yaani kiunganishi.

13. Unapoanza kufanya jambo mwanzoni utakumbana na vitu vingi hasi vitakavyoweza kukukatisha tamaa. Dawa nzuri ya kuepuka kukatishwa tamaa licha ya kukumbana na changamoto ni kuwa kiziwi. Kuwa kiziwi ndio, usisikilize kelele za pembeni lenga mbali katika malengo yako mpaka ufikie juu ya mnara. Kufika juu siyo kazi rahisi lazima ukumbane na vikwazo vitakavyokuimarisha baadaye.

14. Tunaishi katika mazingira ambayo wengi wao ni binadamu. Hapa tunajumuisha watu tunachangamana nao kila siku. Watu hawa wametokea sehemu mbalimbali zenye tamaduni tofauti na historia tofauti. Kila mtu ana uzoefu wa kipekee. Ili kuwajua vizuri watu unatakiwa kujua tofaouti zao na hisia zao katika maisha. Kufanya hivyo kutakupatia nguvu na kupata sensi ya muunganiko. Ukimwelewa mtu ni zaidi ya mawasiliano bora.

15. Kuwa sehemu ya watu. Vaa viatu vyao, yajue matatizo yao,wasikilize maoni yao. Yafanyie kazi maoni yao. Ili uweze kutatua matatizo ya watu kwanza wasikilize na vaa viatu vyao utapata suluhisho zuri. Kusanya maoni kwa watu nayafanyie kazi.

16. Sikiliza mapungufu unayoambiwa, pale unapokosolewa juu ya kitu Fulani . Kukosolewa ni kioo kwako. Tumia kukosolewa kama kioo kwako kwa kuyafanyia kazi na kujiboresha zaidi hatimaye kuwa bora zaidi.

17. Watu wengi huwa hawang’ang’anii kitu mpaka wapate au waone matokeo. Kufanya kitu kwa mguu ndani nje huwezi kupata matokeo mazuri. Unahitaji uwe na shauku na nidhamu ya kusimamia yale yote uliyoyapanga. Kuna watu wanafanya vitu kwa kudonyoa kama vile kuku leo anagusa hiki anaacha kesho hiki anaacha bila hata kupata matokeo. Kwa mtindo huu huwezi kufika mbali. Hivyo simamia kitu unachofanya mpaka upate matokeo.

18. Maisha ya binadamu yako kama vile mtoto anavyojifunza lugha. Sote tumepitia hatua hii ya kujifunza lugha. Mwanzoni tulikuwa tunapata shida katika kujielezea,tunakuwa na shauku na hitaji la kujielezea vile unavyotaka lakini unashindwa yote hii ni kuwa na upungufu wa maneno,taratibu unaanza kujifunza sentensi, misamiati na hatimaye kuwa na uwezo wa kuongea bila kufikiria,kutafuta maneno,bila kusitasita na kunyoa maneno na sentensi unakuwa una flow(fluency). Kujifunza lugha ni hatua au kujifunza kuongea inahusisha hatua ambazo haziepukiki.
Hakuna njia ya mkato katika kujifunza kuongea lugha.
Funzo;
Mafanikio ni safari.
Kila mtu unayemuona amefanikiwa katika sehemu fulani ujue alifuata hatua alianzia chini.
Huhitaji kukurupuka unapotaka kufanikiwa kwa kuona watu wengine wamefanikiwa kiurahisi na wewe utafute mafanikio ya haraka kwa njia za mkato.

19. Kukamilisha kila kitu katika maisha yako inahitaji muda. Unatakiwa uwe mvumilivu katika utafutaji. Una malengo makubwa lakini kuna hatua nyingi njiani unahitaji uzipitie. Tena kuna hatua ndani ya hatua. Hivyo uvumilivu unahitajika.

20. Uhuru siyo kitu ambacho kila mtu anaweza kupewa. Uhuru ni kitu ambacho watu wanaamua kuchukua. Na watu wako huru kama wanavyotaka kuwa.
Hivyo, uhuru katika maisha unajipa mwenyewe hakuna mipaka juu ya hili bali mipaka au kikomo unajipa mwenyewe. Kuwa dira kubwa ya kuwa huru katika maisha yako.

Nakutakia kila la heri rafiki katika haya uliyojifunza leo.

Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: