Huu Ndiyo Aina Ya Msamaha Mgumu Kuliko Wote

Mpendwa Rafiki yangu, Msamaha ni kitu kirahisi kuongea kwa mdomo lakini msamaha ni zaidi ya kuongea kwa mdomo. Ni rahisi kusema nimekusamehe kwa mdomo lakini ndani yako bado unaendelea kubaki na maumivu moyoni. Msamaha wa kweli muda mwingine unatufanya tuonekane wapumbavu mbele za watu. Haiwezakane mtu kusamehewa kosa kama lile, hapa patakuwa na mkono wa …

Jinsi Ya Kuongoza Hata Kama Huna Cheo

Mpendwa rafiki yangu, Kila mmoja wetu ni kiongozi wa maisha yake hilo halina ubishi. Kila mmoja anaendesha maisha yake kadiri anavyotaka yeye na siyo vinginevyo. Tukiwa na nidhamu ya kujisimamia na kujiongoza sisi wenyewe suala la  kuongoza wengine litakua rahisi sana. msingi wa uongozi unaanza na mtu mwenyewe,hapo ulipo unaweza kutengeneza dunia unayotaka. Unaanza kutengeneza …

Hiki Ndiyo Kitu Pekee Ambacho Bado Hujakitoa Hapa Duniani

Mpendwa rafiki yangu, Nina uhakika kabisa kuna kitu ambacho bado hujawahi kukitumia katika maisha yako tokea uzaliwe. Na ingekuwa umekitumia ungeshaanza kupata matokeo ya tofauti katika maisha yako mapema sana. Kila mmoja wetu amezaliwa na upekee wake. Kila mtu ana kitu cha ziada ambacho mtu mwingine hana. Wewe ni maajabu ya ulimwengu, tokea Mungu aumbe …

Kitu Pekee Ambacho Huruhusiwi Kufanya Pale Unapopata Fedha

Mpendwa rafiki, Kila mmoja wetu kila siku anajituma kufanya kazi ili apate kipato kitakachomwezesha kuendesha maisha yake. Wote tunaamini kuwa fedha ndiyo inaendesha maisha yetu, karibu kila eneo la maisha yetu, fedha imetawala na huwezi kuikwepa kwa namna yoyote ile. Ni kweli miongoni mwa watu wengi vipato ni vidogo huku vipato hivyo vikiwa vidogo bado …

Huu Ndiyo Ubora Unaotakiwa Kuonesha Mbele Za Watu

Mpendwa rafiki yangu, Kila mmoja wetu ana ubora na uimra wake. Hakuna mtu anayeweka juhudi kila siku kutafuta udhaifu bali ubora. Kila mmoja wetu anauza ubora, ndiyo maana tunajitahidi kila siku kuwa bora. Ukiitwa kwenye usaili utaulizwa tuambie juu ya ubora wako kwa sababu unaenda pale kuuza ubora yaani ujuzi na muda wako uliokuwa nao …

Hii Ndiyo Sehemu Ambayo Ukombozi Wa Binadamu Unaanzia

Rafiki, Unaweza kutumia akili yako kutatua matatizo ya dunia au unaweza kutumia akili yako kuongeza thamani ya dunia. Unaweza kutumia akili yako kubadilisha maisha yako na yakawa safi kama vile unavyotaka. Sisi binadamu ni binadamu ambao tuna uwezo mkubwa sana. Ukombozi wowote wa binadamu unaanzia kwenye akili. Akili yako ni kiwanda cha maarifa hivyo kadiri …

Hii Ndiyo Faida Moja Pekee Tunayoipata Kupitia Makosa Tunayofanya

Kila mmoja wetu anafanya makosa katika maisha yake.  Hakuna ambaye hakosei kila mtu anakosea na huo ndiyo udhaifu wa binadamu. Tunapofanya makosa iko faida moja ya kipekee sana tunayoipata katika maisha yetu kupitia yale makosa tunayofanya kila siku. Kupitia makosa tunayofanya, inakuwa ni kama shule kwani katika shule tunajifunza mengi ambayo yanatusaidia kuendesha maisha yetu …

Kabla Hujaendelea Na Safari Ya Mafanikio Yako Soma Hapa Kwanza

Kila mmoja wetu anasafiri safari yake ya mafaniki, kila mtu ana njia yake ya kupita kule anakotaka kufika. Lakini kabla hatujaendelea na safari zetu hebu tukae chini tujiulize hili swali. Je uko kwenye njia sahihi? Kama hauko kwenye njia sahihi tafadhali usiendelee kuongeza mwendo. Kwa sababu kuendelea kuongeza mwendo kwenye njia ambayo siyo sahihi ni …

Hivi Ndiyo Vitu Ambavyo Anapoteza Mtu Kabla Hajafanikiwa Kwenye Maisha Yake

Rafiki, Tunapojifunza hadithi za mafanikio huwa tunaangalia na kuona kama mambo ni marahisi tu kama vile unavyosoma hadithi za sungura na fisi. Ila kwa uhalisia kila kitu kinahitaji kazi na tena siyo kazi rahisi gharama yake ni kubwa sana. Ili ufanikiwe lazima ukubali kujitoa sadaka au kafara. Na ninaposema hivyo naamanisha kuwa ni lazima ukubali …

Hii Ndiyo Sababu Inayokufanya Wewe Usifanikiwe

Kila mmoja wetu anapenda kufanikiwa lakini siyo kila mmoja wetu yuko tayari kulipa gharama za mafanikio anayotaka. Kufanikiwa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine, ingekuwa ni rahisi kila mtu angefanikiwa kwa sababu ni ngumu ndiyo maana wachache ndiyo wanafaidi matunda ya mafanikio hapa duniani. Mafanikio yana kazi sana, kwanza tunapotaka mafanikio fulani katika maisha yetu …

Design a site like this with WordPress.com
Get started