Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Sehemu Ambayo Ukombozi Wa Binadamu Unaanzia

Rafiki,

Unaweza kutumia akili yako kutatua matatizo ya dunia au unaweza kutumia akili yako kuongeza thamani ya dunia.

Unaweza kutumia akili yako kubadilisha maisha yako na yakawa safi kama vile unavyotaka. Sisi binadamu ni binadamu ambao tuna uwezo mkubwa sana.

Ukombozi wowote wa binadamu unaanzia kwenye akili. Akili yako ni kiwanda cha maarifa hivyo kadiri unavyoitumia vizuri ndivyo unavyoweza kupata kile unachotaka.

Angalia namna gani dunia inavyopendeza sasa kwa sababu ya watu kutumia akili? Leo hii unasoma huu ujumbe hapa kwa njia ya simu ni matokeo ya binadamu kutumia akili.

Kuna maajabu mengi yanayoendelea kufanyika kila siku kwa kutumia uwezo mkubwa wa akili ambao binadamu anao.

Maisha yako, yako hivyo yalivyo leo kutokana na utumiaji mzuri wa akili. Kama hutumii akili yako vizuri basi utakua unatumia hisia kujiongoza ndiyo maana hufanikiwi.

Hakuna mtu ambaye anaweza kusimama na kutoa ushahidi kuwa alitumia akili yake vizuri ndiyo maana hajafanikiwa.

Ila watu wanaweza kusimama na kusema kuwa hawajafanikiwa kwa sababu hawajatumia akili zao vizuri. Ni hili ni kweli wala halihitaji ushahidi wowote ule.

SOMA; Akili Yako Iwaze Kitu Hiki Ili Uwe Na Mafanikio Makubwa

Kila kitu katika maisha yetu huwa kinaanzia kichwani yaani kwenye akili, huwezi kupata fedha ambazo ulikuwa bado hujajiandaa kupata kiakili.

Utajiri unaanzia kuujenga kwanza ndani ya fikra zako halafu ndiyo unakuja nje.  Duniani kote hakuna mtu masikini, bali kuna akili masikini. Watu wanashindwa kutumia akili zao vizuri ndiyo maana hawapati maisha bora.

Kama unataka maisha ya kawaida tumia akili yako kawaida, kama unataka maisha ya juu na bora tumia akili yako kwa uwezo wa juu.

Unajua akili yako iko raba bendi kadiri unavyoivuta ndivyo inavyovutika. Ni uamuzi wako wewe kutumia kadiri ya urefu unaotaka. Kama vile mbuzi anavyokula kadiri ya urefu wa kamba yake basi binadamu unaishi kadiri utumia mzuri wa akili yako.

Na ili akili yako iwe bora, unatakiwa uwe unailisha maarifa bora kila siku. Kila mtu analisha mwili wake kila siku, lakini siyo wengi wanaolisha akili zao.

Jitahidi kunenepa akili, maana mwili bila akili ni sawa na uko uchi.

Hatua ya kuchukua leo; ilishe akili yako maarifa chanya kila siku. Itumie akili yako vizuri maana uwezo mkubwa wa binadamu uko kwenye akili yake.

Kwahiyo, unapotaka kuwa na maisha fulani anza kwanza kubadili akili yako. Unaalikwa kubadili akili yako ili uweze kubadili maisha yako.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana.

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: