Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kabla Hujaendelea Na Safari Ya Mafanikio Yako Soma Hapa Kwanza

Kila mmoja wetu anasafiri safari yake ya mafaniki, kila mtu ana njia yake ya kupita kule anakotaka kufika. Lakini kabla hatujaendelea na safari zetu hebu tukae chini tujiulize hili swali.

Je uko kwenye njia sahihi? Kama hauko kwenye njia sahihi tafadhali usiendelee kuongeza mwendo. Kwa sababu kuendelea kuongeza mwendo kwenye njia ambayo siyo sahihi ni kupotea njia kabisa.

Kwa mfano, leo umepanda gari lako na kuelekea labda arusha, mara njiani ukaja kushtuka gari ulilopanda siyo sahihi haliendi arusha je utaendelea kusafiri wakati kule unakokwenda siyo sahihi?

Leo jitafakari karibu kila eneo la maisha yako je njia uliyopo ni sahihi? Kama ni sahihi endelea kuchochea mwendo ili uwahi kule unakotaka kufika.

Lakini,

Kama siyo njia sahihi wala usijisumbue tena kuongeza mwendo maana ndiyo utazidi kupoteza maisha yako yote.

Katika maisha ya wanamafanikio huwa wanakuwa na muda wa kujitathimini, kwa siku, mwezi au hata wiki.

Kama maisha yako huyatathimini basi maisha unayoishi hayana maana kuishi hata siku moja. Unapojitafakari ndiyo unapata uelekeo wa maisha je kule unakokweda ni sahihi au siyo sahihi.

SOMA; Kabla Hujalala Leo Hakikisha Unafanya Kitu Hiki Muhimu Kwako

Siku mwanafalsafa mmoja alikuwa anasafiri na wanafunzi wake, mmoja wa wanafunzi akaingia katika nyumba ambayo ilikuwa siyo sahihi, inasemekana nyumba hiyo ilikuwa ni ya watu wanaotenda maovu sana na kufanya maasi makubwa. Sasa mwalimu akamwita ila mwanafunzi aliendelea kujificha kwa aibu ya kuingi mle ndani na kukataa kutoka.

Mwanafalsafa na mwalimu wake akamwambia, kuingia kwenye dhambi siyo kosa, bali kuendelea kubaki kwenye dhambi ndiyo kosa. Hapa tunajifunza nini?

Tunajifunza kuwa kila mtu anakosea na ukishagundua umefanya makosa usione aibu ya kutoka hapo. Kuanza upya siyo ujinga bali kuendelea kufanya ujinga ndiyo ujinga.

Hatua ya kuchukua leo; tafakari mapito yako, kama umejiona uko njia ambayo siyo sahihi toka na nenda njia sahihi.

Kwahiyo, kabla hujaendelea na safari yako, hebu weka kituo leo cha kujitathimini upya ili uwe na mwisho mzuri wa safari na kufika salama kule unakotaka kufika.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana.

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: