Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Faida Moja Pekee Tunayoipata Kupitia Makosa Tunayofanya

Kila mmoja wetu anafanya makosa katika maisha yake.  Hakuna ambaye hakosei kila mtu anakosea na huo ndiyo udhaifu wa binadamu.

Tunapofanya makosa iko faida moja ya kipekee sana tunayoipata katika maisha yetu kupitia yale makosa tunayofanya kila siku.

Kupitia makosa tunayofanya, inakuwa ni kama shule kwani katika shule tunajifunza mengi ambayo yanatusaidia kuendesha maisha yetu kadiri ya sehemu husika.

Maarifa tunayopata yanatusaidia kutupa mwanga eneo fulani ambalo tunakosea. Siyo ujinga kufanya makosa ila katika makosa tunapata kitu ambacho ni KUJIFUNZA.

Katika kosa lolote tunalofanya iwe ni kwa kujua au kwa kutokuja tunapata funzo ndani yake. Katika kila baya huwa kuna zuri ndani yake hivyo unapofanya jambo na ukaona umepata matokeo tofauti kitu unachotakiwa kufanya ni kushukuru na kuondoka na kitu ambacho umejifunza.

Huwa tunachukulia makosa kama ni kitu hasi sana, lakini pale tunapokosea tujaribu kujifunza na kuchukua hatua inayotakiwa.

SOMA; Kosa Kubwa Unalofanya Katika Maisha Yako

Ukishajifunza unaalikwa kuchukua hatua haraka sana ili yasijitokeze mengine. Pia makosa yanatufanya tuwe makini, kama tulifanya kosa kwa uzembe fulani basi hayo makosa yanatufanya tuwe makini sana katika maisha yetu.

Linapotokea kosa tunakumbuka mwanzoni nilifanya vile ikajitokeza hivi hivyo leo sitaki tena kufanya hivi yasije yakatokea tena kitu ambacho siyo. Kama leo umefanya kosa kwa uzembe siku nyingine utakuwa makini.

Kila kitu kinakuja na funzo ndani yake, hivyo unapoona umefanya kosa fulani usikasirike na kujiona wewe ni mzembe sana bali chukua funzo ndani yake na siku nyingine utakua makini.

Hatua ya kuchukua leo; usiogope kukosea, chukulia kila kosa kama funzo katika maisha yako na fanyia kazi kwenye kila kosa unalofanya.

Kwahiyo, makosa ni mwalimu mzuri sana, anatusaidia kutufanya kuwa imara na kuwa bora kila siku. Tunakuwa bora kila siku kwa kujifunza kupitia yale tunayofanya. Hivyo chukua hatua chanya kwenye kila kosa unalofanya sasa.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana.

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: