Kila mmoja wetu anapenda kufanikiwa lakini siyo kila mmoja wetu yuko tayari kulipa gharama za mafanikio anayotaka.
Kufanikiwa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine, ingekuwa ni rahisi kila mtu angefanikiwa kwa sababu ni ngumu ndiyo maana wachache ndiyo wanafaidi matunda ya mafanikio hapa duniani.
Mafanikio yana kazi sana, kwanza tunapotaka mafanikio fulani katika maisha yetu tunaanza kupigana vita. Na vita vya kwanza kwenye mafanikio tunayotaka ni dhidi ya miili yetu. miili inataka tufanye vile inavyotaka na siyo vile tunavyotaka sisi.
Nioneshe mtu aliyefanikiwa kwa jambo lolote lile ambaye hakupata upinzani mkubwa dhidi ya mwili wake. Mfano mzuri ni kuamka asubuhi, kuamka tu asubuhi vita vikubwa sana, mwili hautaki na ukisema uusikilize mwili utasema ni kweli unatakiwa kuusikiliza mwili vile unavyotaka.
KUPATA VITABU VYA KUJISOMEA BONYEZA HAPA
Watu wanaousikiliza mwili vile unavyotaka huwa wanaishia kuwa masikini maisha yao yote.
Sababu moja inayowazuia watu wengi wasifanikiwe kwenye maisha yao ni kuwa kutokuwa bize na maisha yao. Watu wengi wako bize na maisha ya watu wengine kuliko yao. Wako radhi kujua nini kinaendelea kwenye maisha ya wengine kuliko maisha yao binafsi.
SOMA; Sehemu Pekee Ambayo Unapaswa Kuweka Nguvu Zako Ili Upate Mafanikio
Juhudi kubwa zinawekwa kufuatilia mambo yanayoendelea duniani kuliko hata yale malengo ambayo watu wamejiwekea. Watu utakuta wanajadili ajali ambayo tayari imeshatokea na ni kitu kipo nje ya uwezo wao hawawezi kufanya chochote ili kuzuia kile ambacho tayari kimetokea. Maji yakisha mwagika hayazoleki.
Usipoteze muda kuwa bize na mambo ya watu ndiyo maana unasahau ya kwako na ukishasahau mambo yako maana yake huwezi kufanikiwa. Hebu niambie kila siku unaweza kutembelea mitandao ya kijamii hata miwili lakini hapo hapo hujatimiza hata malengo uliyojiwekea ndani ya siku.
Ukikosa kuwa makini na maisha yako maana halisi huna maana ya kuishi hapa duniani. Watu wazembe na wasiyokuwa na nidhamu ya maisha yao ndiyo wanaharibu duniani kila siku. Kuwa makini na maisha yako ili uifanye dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kwa kila mmoja wetu.
Hatua ya kuchukua leo, jipunguzie mzigo wa kufuatilia maisha ya watu, nini kimetokea duniani hebu kuwa bize na maisha yako fanya kile unachotakiwa kufanya ili uishi. Wajibika na maisha yako na siyo mambo ambayo hayakuingizi shilingi.
Kwahiyo,tumia nguvu na muda wako kuwekeza kwenye mambo chanya. Kujadili au kufuatilia vitu ambavyo viko nje ya uwezo wako ni kutaka kuhamisha maji ya bahari utachoka na utashindwa. Dunia umeikuta na utaondoka utaiacha na mambo yake, hivyo itumie vizuri kwa mambo yako ya maana ili ukiondoka uwe huna deni.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.
Leave a comment