Rafiki,
Tunapojifunza hadithi za mafanikio huwa tunaangalia na kuona kama mambo ni marahisi tu kama vile unavyosoma hadithi za sungura na fisi. Ila kwa uhalisia kila kitu kinahitaji kazi na tena siyo kazi rahisi gharama yake ni kubwa sana.
Ili ufanikiwe lazima ukubali kujitoa sadaka au kafara. Na ninaposema hivyo naamanisha kuwa ni lazima ukubali kupoteza vitu au kitu kizuri ili upate kitu bora. Lazima ukubali kuachia kitu kimoja ili uweze kupata kingine lakini huwezi kuondoka navyo vyote kwa pamoja.
Ninaposema kafara siyo kafara za kishirikina, kwa mfano, kwa wale wanaoamini dini zao wako wale viongozi wao kama vile Yesu na Mohamad waliweza kujitoa kafara juu ya dini zao, kama Yesu alijitoa kafara kwa kuteswa msabani ili watu wake wakombolewe. Unaona kitu kinachoitwa mafanikio ni msamiati unaohitaji kazi kweli kwa maneno huwezi ila kwa vitendo na kujitoa kafara lazima utaweza tu.
Mpaka unamuona mtu amefanikiwa jua kabisa hapo mwanzo alipoteza vitu vingi sana. wapo wanaopoteza vitu vingi sana kabla hawajafanikiwa. Wako wanaopoteza fedha nyingi kwa kujaribu vitu vingi kabla hawajafanikiwa.
Unapomuona mtu amesimama eneo fulani ujue kabisa alijitoa kafara kupitia eneo hilo siyo kazi rahisi. Watu wanatumia nguvu, muda na fedha kujaribu vitu vingi ili waweze kutimiza ndoto zao.
Hivyo unapomuona mtu amefanikiwa jifunze kuwa kuna mengi ambayo alijaribu sana na akashindwa na ujue amepoteza fedha nyingi sana mpaka kufikia hapo alipo leo.
Kama unataka kufanikiwa jitoe mhanga kwenye kile unachotaka. Mtaka cha uvunguni sharti ainame. Usitegemee utapata kile unachotaka chini ya uvungu huku ukiwa umesimama.
SOMA; Hii Ndiyo Sababu Inayokufanya Wewe Usifanikiwe
Tunapaswa kuwa wanyenyekevu kama falsafa ya ufagio inavyotualika. Falsafa ya ufagio ni unyenyekevu lazima uiname pale unapotaka kufagia hata uwe nani kwenye ufagio lazima uwe mpole. Hivyo yaendee mafanikio kwa namna hiyo tii kila kinachohitaji ili uweze kupata kila unachotaka.
Hatua ya kuchukua leo; kila kitu kimelipiwa gharama. Hivyo chochote kile unachotaka kwenye maisha yako kuwa tayari kujitoa sadaka au kafara ili uweze kukipata. Yaani jitoe kweli kwenye kile unachotaka bila kujali sababu fulani na utafanikiwa.
Kwahiyo, mafanikio yako tu kwa wale wanayoyatafuta na kuyavumilia mpaka wayapate. Usitegemee mafanikio yatakufuata hapo ulipo bali wewe ndiyo uyafuate.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.