Mafanikio Mengi Ya Kifedha Huwa Yanakuja Na Hili Pia

Mwanamziki wa kimarekani Rick Ross kwenye moja ya wimbo wake mmoja anasema fedha nyingi, matatizo mengi, usiniite bosi yaani more money, more problem don't call me the boss. Mafanikio ya kifedha huwa yanakuja na matatizo makubwa ya kifedha pia. Siyo kwamba ukishakuwa na fedha nyingi ndiyo umeshayapatia maisha yako, yaani huhitaji tena kuhangaika hapana, siyo …

Ifanye Siku Ya Mwenzako Kuwa Bora Kupitia Hiki Hapa

Huwezi kuishiwa pale unapotoa thamani kubwa kwa wengine. Kwa mfano, watu wanakula samaki kila siku lakini ulishawahi kusikia samaki wameisha baharini? Ifanye siku ya mwenzako kuwa bora kupitia kile unachofanya.Kile unachofanya kina msaidia mwenzako kuwa bora kwa namna moja au nyingine. Kuna watu wanakutegemea kupitia kile ambacho, hata kama huoni mrejesho wake, lakini jua kuna …

Rudia Tena Kufanya

Karibu kila mtanzania anajua kuimba wimbo wa Taifa bila shida yoyote ile. Na watu wanaweza kuimba wimbo wa Taifa kwa sababu walivyokuwa shuleni walikuwa wanauimba karibu kila siku. Hii imepelekea hata watu wengi kuunasa kichwani na kuuelewa bila shida. Hapa tunajifunza kitu kikubwa sana, ukitaka watu wakielewe kitu, unapaswa kukirudia rudia kitu mara kwa mara …

Hii Ndiyo Sehemu Pekee Ya Kupaki Fedha Zako

Kama una fedha nyingi halafu umeziweka benki basi utakuwa hujitendei haki. Unapaswa kuwa na akaunti ya mfuko wa uwekezaji kwa hapa Tanzania tunao mfuko wenye dhamana hiyo unaojulikana kama UTT AMIS. Kuna faida ya kuweka fedha zako kwenye mfuko wa UTT AMIS kuliko kuweka fedha benki. Kwa nini ? Kwa sababu, benki fedha haizalishi zaidi …

Usiishi Bila Kuwa Na “Target”

Kwenye kila eneo la maisha yako unapaswa kuishi kwa "target". Jiwekee target, kwanini ujiwekee target? Kwa sababu tageti inakusaidia kukusukuma na kukuwajibisha ili ufikie malengo yako. Kwenye kazi jiwekee ufikie tageti fulani yaani lengo fulani ufikie. Kwenye eneo la kifedha, jiwekee tageti kwamba kwa mwezi unapaswa kuingiza kipato kiasi fulani. Na ukishaweka tageti pambania kufikia …

Njia Rahisi Ya Kujifunza Mambo Mengi

Ingia kwenye biashara. Kwenye biashara ndiyo chuo cha maisha hakika utajifunza mambo mengi. Utajifunza kuhusu maisha, uongozi, kuhusu ushawishi, kuhusu masoko, mauzo na hata tabia za watu maana utakutana na watu wa tofauti kila siku. Hata kama hutaki kujifunza utalazimika kujifunza kwa sababu unatakutana na vitu ambavyo huvijui. Hutakiwi kusema unajifunza biashara bali ingia kwenye …

Tatizo Linaanzia Kwenye Hisia

Mara nyingi watu huwa wanapanga wataweka akiba wakiwa kwenye akili ya kawaida au hali tulivu kabisa. Na hapo akili zinakuwa zinafanya kazi vizuri. Lakini pale tunapokuwa na fedha na kuona vile vitu tunavyopenda akili zetu huwa zinaruka. Hapo hisia zinakuwa juu kweli na fikra zinakuwa chini mtu anakuwa hakumbuki hata ile mipango aliyokuwa amepanga. Hisia …

Karibu Usome Ushuhuda Huu Wa Kweli Na Kisha Upate Hamasa Na Kuchukua Hatua

Mpendwa rafiki yangu, Mwaka jana Julai 18, ilikuwa ni siku yangu ya kuzaliwa, hivyo kama ilivyo utaratibu wangu ni kufanya tathmini na kushirikisha malengo makubwa niliyonayo ili na watu wengine wapate kujifunza. Katika kumbukizi hiyo ya kuzaliwa nilipata mirejesho mbalimbali leo nimeona nikushirikishe na wewe rafiki yangu ili uweze kupata kujifunza na kuchukua hatua. Ninayo …

Huu Ndiyo Upande Wa Kuzingatia Kama Unataka Kitu Chako Kisomwe

Februari 28 tuliyojifunza bidhaa inayonunulia sana ni ile ambayo iko usawa wa macho. Tulijifunza kwamba ni ngumu mtu kuinama na kutafuta bidhaa au kuangalia juu kutafuta vitu. Watu wanapenda urahisi, hawapendi kujisumbua hivyo basi, watakachoona kitu ambacho kipo usawa wa macho yao ndiyo wanashughulika nalo. Leo napenda kukuongea mbinu nyingine ya mauzo, kama unaandaa tangazo …

Ijue Biashara Na Huduma Ninayotoa Ambayo Ni Suluhisho La Matatizo Yako

Habari rafiki yangu, Nashukuru sana kwa kuendelea kuwa shabiki wa kazi zangu zinazoendelea kuzitoa. Naomba nikukumbushe kuhusu huduma yangu ninayoitoa ya kuuza maarifa kwa njia ya vitabu, makala na huduma ya Mimi Ni Mshindi. Mpaka sasa vitabu ambavyo viko sokoni na bei yake ni kama vifuatavyo; Hivi ni vitabu vya soft copy; 1. Funga na …

Design a site like this with WordPress.com
Get started