Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usiishi Bila Kuwa Na “Target”

Kwenye kila eneo la maisha yako unapaswa kuishi kwa “target”.

Jiwekee target, kwanini ujiwekee target? Kwa sababu tageti inakusaidia kukusukuma na kukuwajibisha ili ufikie malengo yako.

Kwenye kazi jiwekee ufikie tageti fulani yaani lengo fulani ufikie.

Kwenye eneo la kifedha, jiwekee tageti kwamba kwa mwezi unapaswa kuingiza kipato kiasi fulani. Na ukishaweka tageti pambania kufikia malengo yako.

Kwenye biashara yako, weka malengo au tageti yako ni kuwa na mauzo kiasi fulani kwa siku. Na ujisukume namna ya kupata wateja hao ili wakusaidie kutimiza malengo uliyojiwekea.

Weka tageti ya uzalishaji kama unazalisha bidhaa fulani, kwa mfano, kama unazalisha bidhaa kama keki, weka tageti kwamba kwa siku kwenye kiwanda chako unatakiwa uzalishe keki ngapi.

Bila kuwa na tageti ni ngumu kujisukuma. Watu wengi ambao hawana tageti ya kitu fulani huwa hawana hata mwamko wa kujituma.

Kama umejiajiri jipe tageti ya kufikia kitu fulani. Kama umeajiriwa jiwekee tageti na kimbizana kukamilisha tageti yako. Wawekee wasaidizi wako wa kazi kufikia malengo fulani kila siku.

Mke na mume kuweni na tageti ya kufikia malengo yenu.

Watoto wapewe malengo ya kufanyia kazi na wapambane kuyafikia malengo hayo.

Kama wewe ni mwalimu wape tageti wanafunzi wako, waambie unataka matokeo ya aina gani na wajitume kweli kuyafikia malengo hayo. Bila kuwapa malengo, watakua wanapata matokeo ya kawaida tu.

Kama wewe kazi yako ni kuponya roho za watu kama askofu, padre, mchungaji, mwinjilisti au katekista, sista, braza, shehe, mufti, maalimu,nk hakikisha unakuwa na tageti ya namna ya kuwasaidia wale unao wahudumia kiroho.
Wape tageti wale unaohudumia kiroho na fuatilia kuhakikisha wanafikia tageti uliyojiwekea.

Hatua ya kuchukua leo; kwenye kila eneo la maisha yako jiwekee tageti na hamasika na jisukume kuyafikia malengo hayo.

Usikubali kuishi bila kuwa na tageti ya kitu fulani. Usipojipa tageti, asili itakutumia kwenye mambo ambayo hata hukupanga, au utapata hata matokeo ambayo huyataki.

Weka tageti ili asili ijue wewe unataka nini, maana usiposema utaweza kupewa usichostahili kupata.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: