Design a site like this with WordPress.com
Get started

Huu Ndiyo Upande Wa Kuzingatia Kama Unataka Kitu Chako Kisomwe

Februari 28 tuliyojifunza bidhaa inayonunulia sana ni ile ambayo iko usawa wa macho. Tulijifunza kwamba ni ngumu mtu kuinama na kutafuta bidhaa au kuangalia juu kutafuta vitu. Watu wanapenda urahisi, hawapendi kujisumbua hivyo basi, watakachoona kitu ambacho kipo usawa wa macho yao ndiyo wanashughulika nalo.

Leo napenda kukuongea mbinu nyingine ya mauzo, kama unaandaa tangazo lako la biashara au kitu chochote kile weka upande wa kulia.

Kwa sababu, kitu ambacho kipo upande wa kulia huwa kinasomwa sana kuliko vitu vya kushoto. Kwa mfano, gazeti, tangazo lililokaa upande wa kulia linasomwa sana ukilinganisha na kushoto.

Hujawahi kujiuliza ni kwanini hata mwalimu wako darasani alikuwa anaandika tarehe upande wa kulia? Kwenye taaluma ya ualimu, unafundishwa unapaswa kuandika tarehe ubaoni upande wa kulia.

Kama ulikuwa hujui sasa pata kujua leo, wanafanya hivyo kwa sababu upande wa kulia huwa watu ndiyo wanasoma sana na rahisi kuona kuliko kushoto.

Mpaka hapa umeshapata mbinu mbili za kutangaza biashara au kile unachotaka watu wakijue yaani masoko.

Masoko ni kuiwezesha biashara yako kujulikana hivyo ukitumia njia ya kuweka bidhaa zako usawa wa macho na ukitumia upande wa kulia ambao watu wanaona sana itakusaidia kufanya masoko kwenye biashara yako.

Kama unaandaa tangazo lako na unataka watu wasome kwenye eneo husika liweke upande wa kulia ndiyo watu huwa wanasoma sana vitu vilivyokuwa upande wa kulia.

Hatua ya kuchukua leo; Teka umakini wa mteja wako kwa kumwekea bidhaa unazotaka zitoke haraka upande wa kulia lakini pia usisahau kuweka bidhaa usawa wa macho.

Kumbuka, bidhaa inayonunulia sana ni ile ambayo iko usawa wa macho katika biashara unayofanya, mteja akija hakikisha bidhaa unazotaka ziende mwekee usawa wa macho na ukitaka hata kitu kisomwe sana au kionekane kama tangazo lako liweke upande wa kulia.
Matangazo ambayo yanasomwa sana mengi utakuta yamebandikwa usawa wa macho na upande wa kulia. Hivyo hii ni mbinu ya kisaikolojia ambayo itakusaidia katika huduma unazotoa.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: