Njia Rahisi Ya Watu Kukupuuza

Sisi binadamu ni rahisi sana watu kutupuuza kama kuna kitu ambacho tulishakijenga ndani yetu halafu tukashindwa kukitekeleza. Kwenye maisha tunaalikwa kuwa tuishi kile ambacho tunakisema. Na hapa tunakuwa tunaishi falsafa hii, ahidi makubwa na tekeleza makubwa. Watu wengi wamekuwa siyo waaminifu, wanaahidi tu lakini hawatekelezi. Watu huwa wanatupuuza pale ambapo tunakuwa tumeahidi halafu tumeshindwa kutekeleza …

Wape Watu Mrejesho

Mrejesho ni zawadi. Kila mmoja wetu anapenda kupokea mrejesho wa kile ambacho amefanya au kusikia mrejesho kutoka kwa wale ambao amewafanyia kitu. Lakini watu wengi hawana ustaarabu kwenye maisha. Watu hawatoi mrejesho na unashindwa kujua kama kile ulichotoa au kimemsaidiaje.Watu wanahitaji mrejesho kwenye kila eneo la maisha yetu. Na mrejesho ni zawadi kwa kila mmoja …

Jinsi Ya Kuwashawishi Watu Kufanya Kitu

Mpendwa rafiki yangu, ukitaka kuwashawishi watu, wape watu maana na watakuwa tayari kufanya kitu hiko haya kwa gharama ndogo. Watu wanapenda kufanya kitu chenye maana kwao na kwa wengine hata kama hawapati malipo makubwa. Kwa mfano, watu wanaweza wakajituma sana kwenye kazi za kusaidia kuliko hata kazi wanazolipwa. Unajua ni kwa nini? Hii ni kwa …

Lenga Jitihada Zako Zote Hapa Na Utafanikiwa

Huwa tunajua kwamba mtu akitawanya nguvu ndiyo anafanikiwa. Yule mtu anayejaribu vitu vingi ndiyo anaonekana mjanja kuliko yule anayeshughulika na kitu kimoja. Waswahili wanasema, mshika mawili moja, humponyoka. Hivyo basi, kama mtu akiweka nguvu zake kwenye kitu kimoja ataweza kufanikiwa zaidi. Ili uweze kufanikiwa kwenye jambo lolote lile, kwanza lenga Jitihada zako zote sehemu moja.Amua …

Haya Ndiyo Matumizi Matatu Ya Fedha

Fedha ni jawabu la mambo yote. Hilo halina ubishi kwani inakubalika kila eneo la maisha yetu. Mwandishi wa kitabu cha Total Money Makeover mwandishi Dave Ramsey amesema kwamba, fedha ina matumizi matatu na matumizi hayo ni kama ifuatavyo. Moja, kufurahia maisha.Je, unafurahia maisha yako?Hakuna maana kukazana upate fedha nyingi halafu ushindwe kuyafurahia maisha yako. Unapaswa …

Kushiriki Kikamilifu Na Kutaka Kuonekana

Kwenye matukio ambayo watu wengi wanashiriki, wengi wanakuwepo kwa madhumuni mawili.Moja, mwingine anashiriki kwenye jambo ili tu apate kuonekana kwamba ameshiriki.Na mwingine anashiriki kwenye jambo kikamilifu. Kushiriki kikamilifu maana yake akili yako yote inakuwa pale na kutekeleza yale yanayopaswa kufanywa kadiri ya mahitaji ya tukio. Kwa mfano, kuhudhuria nyumba za ibada, wako ambao wanaenda nyumba …

Maisha Ni Mahusiano

Ili uweze kufanikiwa kwenye jambo lolote lile, unahitaji watu watakaokuwezesha kufanikisha jambo lako. Watu ambao watakuja kwenye jambo lako lolote lile, ni wale ambao umehusiana nao. Kwa mfano, unaenda kwenye harusi, send off ambayo tayari una mahusiano na wale ambao mnahusiana nao. Vitu vingi ambavyo vinatupita ni vile ambavyo hatuna mahusiano navyo. Kama unahusiana na …

Haya Ndiyo Mawazo Unayopaswa Kuyafikiria

Kila siku unapaswa kufikiria mawazo ya kujenga.Na kile unachofikiri ndiyo kinaamua ni nini utafanya. Kila unachofikiri kila mara ndiyo kitaamua ni wapi utakapoishia na maisha yako. Hii ndiyo sababu kubwa kwa nini ni muhimu sana wewe kushirikiana na watu wenye mawazo ya mafanikio. Tengeneza timu ambayo mtashirikiana na kusaidiana, utajitengenezea uhakika wa kufanikiwa. Maandalizi makubwa …

Vunja Tabia Mbaya

Ukivunja tamaa, unaweza kuondokana na tabia mbaya.Unafikiri nini kinachowafanya watu wengi kuendelea na tabia mbaya? Kinachowafanya watu wengi kuendelea na tabia mbaya ni kushindwa kuzuia tamaa zao, hasa pale zinapokuja kwa nguvu kubwa. Pale unaposalimu amri kwa tamaa zako ndiyo kitu kinachofanya tabia mbaya kuendelea kuwepo. Vunja tabia zinazokupelekea kwenye uraibu. Uraibu wa kukupeleka kwenye …

Wakikupa Hela, Watakupangia Hiki

Hapa duniani kila binadamu yuko katika maslahi yake binafsi.Watu huwa wanaangalia wanapata nini kwanza ndiyo wafanye kitu. Ni asili ya kila binadamu kuwa mbinafsi. Anaangalia kwanza yeye atapata nini. Ukiona mtu anafanya kitu, jua kuna maslahi binafsi anapata. Kwenye maisha unapaswa kuwa makini, watu wakikupa hela, basi watakupangia cha kufanya. Unakuwa mtumwa kwa watu hao. …

Design a site like this with WordPress.com
Get started