Usimkatie Mtu Tamaa

Kwenye maisha huwa tunawakatia tamaa watu wengi ambao tunahusiana nao. Tunawakatia tamaa na kuona kama vile wamefikia mwisho.Kuwakatia watu tamaa maana yake ni kama kuwawekea nukta kwamba hawawezi tena kuendelea. Tumegeuka kuwa miungu watu wa kuwawekea watu ukomo.Tunaona watu hawawezi kumbe wanaweza.Yako maeneo mengi ambayo tumewakatia watu tamaa kwenye maisha yao. Tunaona hawawezi tena.Kila mtu …

Njia Nzuri Ya Kutopuuzwa

Kila mtu anapenda kufanya kitu na kuonekana yuko vizuri. Ni jambo zuri kufanya kitu na kuonekana uko vizuri. Kama unataka usipuuzwe kwenye kitu chochote kile, kwanza fanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Ukiwa bora, hakuna atakayekupuuza hata siku moja.Mtu ambaye anafanya vitu vyake hovyo hovyo, mara nyingi huwa anapuuzwa. Na kitu kingine ni …

Ufukara Siyo Kilema

Kwenye maisha kuna vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wako na kuna vitu ambavyo viko nje ya uwezo wako.Kuzaliwa masikini siyo kosa lako ila kufa masikini ndiyo kosa lako. Kama umezaliwa masikini, unapaswa kupambana kiasi kwamba ile hali ya umasikini iondoke kwako.Laana ya umasikini inaondolewa na kitu kimoja tu, nacho ni KAZI. Kama umasikini ni …

Kabla Ya Kutaka Kuongea, Jiulize Swali Hili Hapa

Mwanaidi Plato aliwahi kunukuliwa akisema, werevu huongea kwa sababu wana kitu cha kuongeza. Ila wapumbavu huongea kwa sababu inabidi waseme kitu. Wakati wowote ule unapotaka kuongea, jiulize swali hili,Jiulize je, una kitu cha kuongea au na wewe unataka usikike tu kwamba umeongea? Kwa kufanya hivyo, itakusaidia kujizuia kuongea mambo ambayo siyo ya muhimu. Kama huna …

Njia Bora Kabisa Ya Kuwaadhibu Wale Wenye Chuki Na Wewe

Ni kawaida ya binadamu kuchukiwa. Hakuna mtu ambaye hachukiwi kwa sababu kila anayeenda hatua ya ziada wale ambao hawapendi maendeleo yao lazima watawaonea wivu. Watu hawapendi kuonekana wameshindwa, watu hawapendi kuonekana wao ni wavivu au wazembe. Kinachotokea ni kwamba, kukufanya wewe usifikie ndoto zako ili muwe sawa. Wapo watu ambao watakuchukia kwa sababu ya mafanikio …

Kigeuze Hiki Ili Kikuletee Fedha

Kwa chochote kile unachopenda kufanya sasa unaweza kukigeuza kuwa sehemu yako ya mafanikio. Unaweza kukigeuza kuwa sehemu ya dunia kukujua wewe kupitia kile unachofanya. Kuwa sehemu ya kutoa thamani kwa wengine na kufanya makubwa sana. Kama unakipaji, usife njaa kitumie kukuingizia fedha. Au chochote unachopendelea kukifuatilia, angalia ni namna gani unaweza kuongeza thamani kwa wengine …

Lazima Sababu Itokee

Hakuna jambo ambalo litatokea kwenye maisha yako bila sababu. Kwa mfano, ukichukua jiwe na kuliweka ndani haliwezi kuondoka hapo mpaka mtu aje alihamishe. Ili upate matokeo fulani kwenye maisha yako, lazima kuwe na sababu yaani kisababishi. Sheria ya sababu na matokeo(laws of cause and effects) ndiyo inayoendesha dunia. Hakuna kinachotokea bila sababu. Kwa mfano, hakuna …

Ushindani Wa Kijinga Kwenye Biashara

Kila mtu anataka kuuza zaidi kwenye biashara yake. Na pale mtu anapoona hauzi huwa anafikiria namna ya kuweza kufanya ili aweze kupata wateja. Sasa ujinga ambao wanafanya wafanyabiashara wengi pale ambao anaona hauzi ni kushusha bei.Watu wengi siku hizi wanajiita vunja bei wakiwa na imani kwamba wakipunguza bei watapata wateja wengi zaidi. Kama una biashara, …

Unachotakiwa Kujua Ni Hiki Hapa

Bilionea na mshirika mwenza wa Warren Buffett Bilionea Charlie Munger aliwahi kunukuliwa akisema,Ninachotaka kujua ni wapi nikienda nitakufa ili niepuke kwenda sehemu hiyo. Rafiki yangu nikupendaye, tafsiri rahisi ni kwamba jua ni mambo gani ukiyafanya utakufa na kisha acha kufanya kitu hicho. Kwenye kila eneo la maisha yetu kuna vifo. Vifo siyo tu vya binadamu …

Design a site like this with WordPress.com
Get started