Usitumie Ujinga Wa Mteja Kumuibia

Kama unawaza kupata fedha nyingi, basi usifikirie kutumia ujinga wa mteja wako kumuibia kwa sababu hajui. Badala yake unatakiwa kuwa mwaminifu kumsaidia mteja wako kuokoa fedha. Lengo la kila biashara ni kumsaidia mteja kuokoa fedha kwa mfano, ukimuuzia mteja kizuri ambacho kitadumu utamwokolea fedha lakini ukimtapeli unakuwa umemuongezea gharama. Hata kama mteja hana uelewa kwenye …

Swali Muhimu La Kujiuliza Pale Unapoambiwa Kuna Dili La Kupiga Fedha

Kila siku tunasikia madili ya fursa ya kupiga fedha. Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini wanatangaza kwa wengine? Kama ni dili la kupiga fedha kwanini wasizipige wao hizo fedha? Ni nani ambaye hapendi fedha? Ukishaona mtu anakuambia kuna dili la kupiga fedha jua wewe mwenyewe ndiyo dili lenyewe. Ukiona hamna wa kutapeliwa jua wewe ndiyo wakutapeliwa, …

Hatua Ya Kuchukua Pale Unaposhindwa Kitu

Kaa pembeni na waachie wale wanaoweza kufanya wafanye. Ukiona umeshindwa kitu, siyo kwamba kila mtu ameshindwa. Wako ambao wanaona kitu fulani ni kigumu na kwa sababu wao wameshindwa wanaona wote wanaweza kushindwa pia. Kama wewe ni kiongozi sehemu fulani na unaona kabisa uwezo wako umefikia kikomo kaa pembeni waachie wengine. Unapotoa nafasi kwa wengine wanaweza …

Mtaji Ambao Watu Wengi Hawana

Ni mtaji wa uzoefu. Watu wengi hawana mtaji wa uzoefu licha ya kuwa na fedha. Mtaji wa uzoefu ni mtaji ambao una nguvu sana. Ni mtaji ambao utakusaidia kwenda mbele katika biashara, kazi au kitu chochote kile. Kwenye ndoa watu wanahitaji mtaji wa uzoefu. Kwenye biashara watu wanahitaji mtaji wa uzoefu.Kwenye kazi watu wanahitaji mtaji …

Hili Ndilo Sharti Namba Moja La Msamaha

Watu wanakosea namna ya kuombana msamaha hii inawasababisha watu kubaki na manung'uniko, chuki na hasira ndani ya mioyo yao. Kusema naomba msamaha peke yake, bado hujamaliza kiu ya yule uliyemkosea. Kila anayeombwa msamaha kuna sauti ambayo anataka kuisikia kutoka kwa yule aliyemkosea. Kwenye mahusiano yetu migogoro haiishi kwa sababu ya namna watu wanavyoombana msamaha. Mtu …

Hii Ndiyo Siri Ya Kushinda Kwenye Chochote Kile Unachotaka

Wengi wanachagua kushindwa kabla hata hawajaanza kufanya. Watu wanakuwa na mawazo mazuri sana lakini cha ajabu hawachukui hatua mpaka wanaibua hofu ndani yao ya kuzalisha matokeo ya kushindwa. Huwezi kushinda kama hauko tayari kujaribu. Na siri ya ushindi kwenye kitu chochote kile ni kujaribu. Wale ambao unaona wana bahati sana huwa ni watu wazuri sana …

Design a site like this with WordPress.com
Get started