Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Siri Ya Kushinda Kwenye Chochote Kile Unachotaka

Wengi wanachagua kushindwa kabla hata hawajaanza kufanya. Watu wanakuwa na mawazo mazuri sana lakini cha ajabu hawachukui hatua mpaka wanaibua hofu ndani yao ya kuzalisha matokeo ya kushindwa.

Huwezi kushinda kama hauko tayari kujaribu. Na siri ya ushindi kwenye kitu chochote kile ni kujaribu. Wale ambao unaona wana bahati sana huwa ni watu wazuri sana wa kujaribu. Kila wazo alilonalo anajaribu kwa vitendo na kufanya maamuzi kisha kuweka ung’ang’anizi mpaka anakipata kweli.

Siri ya ushindi ni kujaribu. Peleka bidhaa sokoni na soko litaamua lenyewe. Acha tabia ya kulisemea soko, kama una bidhaa ambayo unajua ni suluhisho kwa watu, ipeleke sokoni na watu wenye njaa watakua tayari kulipa gharama ya kile wanachotaka.

Ni dhambi kukumbatia mawazo ambayo hata huyafanyii kazi. Unajinyima bahati yako kwa sababu ya kutokuchukua hatua. Jaribu kushusha nyavu mpaka chini huwezi kukosa samaki. Ni bora kujaribu kuliko kukaa bila kujaribu.

Kwa wazo lolote bora na kubwa ulilo nalo, chagua kuanza namna ya kulitekeleza hata kama ni kwa hatua ndogo. Chagua kuwa mtu wa kujaribu kwa kile kilichopo ndani yako na utashangaa unavyojikutanisha na bahati yako.

Hatua ya kuchukua leo; usikubali kupoteza mawazo mazuri uliyokuwa nayo, badala yake chukua hatua na hautabaki kama ulivyo.

Huna cha kupoteza, fanya kazi yako na asili itafanya kazi yake.
Nakusihi sana kama una wazo lako basi nenda kawe mtu wa kujaribu. Ukitaka kuwa mshindi basi kuwa mtu wa kujaribu kila wazo ulilokuwa nalo.

Leo nenda kajaribu kile unachotaka kufanya na usijali kuhusu matokeo utakayopata. Kaondoe laana ya kutokuanza na kujaribu mawazo yako. Usipoifanyia kazi utajuaje kama inafanya kazi?

Muhimu;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: