Sababu Kuu Moja Kwa Nini Umchukulie Kila Mtu Kwa Heshima

Sisi ni binadamu na maisha yetu kwa asilimia kubwa yanawategemea wengine. Kile ambayo tunahangaika kukitafuta tayari kipo kwa wengine. Mafanikio yote tunayotaka tunapata kwa watu wengine. Hivyo basi watu ni rasilimali muhimu sana.Mchukulie kila mtu unayekutana naye kwa adabu na heshima kwa sababu huwezi kujua ni wakati gani utamwitaji sana kwenye maisha yako. Kila mtu …

Huu Ndiyo Msingi Mkuu Wa Kupata Fedha Duniani

Unaweza kumuona mwenzako anapiga hela eneo fulani na wewe ukaiga ukaenda kufanya huenda hata usipate kama anavyopata yeye. Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini katika timu ya mpira au hata makazini watu wanalipwa tofauti?Wote mnafanya kitu kimoja lakini kila mtu analipwa fedha tofauti? Fedha ni muhimu sana kwenye maisha yetu hilo halina kabisa ubishi. Ni jawabu …

Kushindwa Kitu Ambacho Kipo Ndani Ya Uwezo Wako

Huo ni uzembe mkubwa. Usikubali kushindwa kwa kitu ambacho tayari unao uwezo wa kila namna kukishinda.. Unapopata nafasi yoyote ile, itumie vizuri kwa sababu usipoitumia nafasi ambayo iko ndani ya uwezo wako baadae itakuja kukutesa sana kisaikolojia. Utaanza kujilaumu laiti ningelijua, usikubali upitie maumivu ya laiti ningelijua kwa ni fedheha kubwa kwako. Kama unaweza kushinda, …

Utajiri Muhimu Utakaobaki Na Wewe Mpaka Mwisho

Ni utajiri wa familia na marafiki. Pale mwili na roho yako inapotaka kujitenganisha hutatamani kupata muda wa kufanya kazi zaidi kwenye kile unachofanya au biashara unayofanya. Lakini, utatamani sana kama ungepata muda zaidi wa kuwa na wale watu wako wa karibu unaowapenda. Kwa sababu kila mmoja wetu ametokea katika familia na ataondokea katika familia. Ni …

Mambo Matatu Ya Kufanya Dhidi Ya Mshindani Wako Kibiashara

Katika ushindani wa kibiashara, usipokuwa makini utajikuta na wewe unakimbia mbio za panya na hata ukishinda utabaki kuwa panya. Kwenye ushindani wa kibiashara fanya kile ambacho mshindani wako hafanyi. Hii ndiyo njia bora kabisa ya kushindana kwa sababu haitokuumiza, badala ya kuwa kama yeye, wewe unakomaa kuwa kama wewe. Unakuwa bora sana kwenye kile unachofanya …

Maswali Mawili Yanayochokoza Fikra Za Uvumbuzi

Dunia isingekuwa hivi ilivyo leo kama watu wasingekuwa wanafanya uvumbuzi. Dunia inazidi kuwa bora kwa sababu watu wanazidi kuvumbua vitu vipya kila siku. Uvumbuzi unasaidia maisha ya watu kuwa bora. Leo nimekuandalia maswali mawili yanayokwenda kuchokoza fikra za kivumbuzi ndani yako. Swali namba moja, Kwa nini. Kila unapokutana na kitu mbele yako jiulize kwa nini.Ukiwa …

Design a site like this with WordPress.com
Get started