Kama Inavumilika, Vumilia

Aliyekuwa mtawala wa Roma na mwanafalsafa wa ustoa mwanafalsafa Marcus Aurelius enzi za uhai wake aliwahi kunukuliwa akisema, kama inavumilika, vumilia ila usilalamike. Kama unapitia magumu ambayo yanavumilika vumilia lakini usilalamike. Kama unaona maisha unayoishi si mazuri chukua hatua na siyo kulalamika. Maajabu yanakuja pale ambapo mtu anaendelea kumilia huku akiwa hachukui hatua sahihi badala …

Vitu Viwili Unavyopaswa Kuwa Navyo Ili Ufanikiwe

Siyo kwamba watu hawajui kile wanachopaswa kufanya, ila watu hawana ujasiri wa kufanya kile wanachopaswa kufanya. Kama kila mtu angekuwa na ujasiri wa kusimamia malengo yake basi tungezidi kuiona dunia inazidi kuwa sehemu salama ya kuishi kwa kila mmoja wetu. Ili ufanikiwe kwenye kitu chochote kile kuwa na vitu hivi viwili. Moja, maamuzi. Kama huendi …

Tafadhali, Usirudie Kusema Kauli Hii Tena

Huwezi kufanikiwa kwa makubwa kama madogo unayadharau. Kama unafanya kazi isiyokulipa vile unavyotaka wewe isiwe tiketi kwako kufanya kwa kiwango cha chini. Kazi yoyote iwe inakulipa au haikulipi unatakiwa kuifanya kwa ubora. Kwa sababu kama utashindwa kufanya kazi ndogo kwa ubora hata ukipata kubwa hutafanya kwa ubora. Binadamu tumekuwa ni watu wa kutengeneza tabia na …

Fanya Mambo Haya Mawili Ili Uweze Kuishi Kwa Amani

Amani ni kitu kidogo tu lakini kikikosekana sehemu yoyote panakuwa ni shida. Ukikosa amani nyumbani, kazini, kwenye biashara, mahusiano nk hali inakuwa mbaya. Tunapokwenda kuabudu kwenye nyumba zetu za ibada tunahubiriwa amani, na wakati tukitaka kuondoka tunaambiwa amani ya Bwana iwe nasi na tuende kwa amani. Kumbe basi, amani ikiwepo kila kitu kitakuwepo. Kama hakuna …

Huyu Ndiye Msemaji Mkuu Wa Maisha Yako

Kwenye taasisi nyingi huwa kuna msemaji mkuu wa taasisi hiyo. Siyo kila mtu ni msemaji maana kuna watu wengine wakisema wanaweza kuharibu kabisa hali ya hewa badala ya kusaidia. Kama kila mtu akiwa ni msemaji mkuu, kutakuwa na fujo nyingi. Mwingine anaweza kujiuliza sasa kama mimi sina msemaji mkuu wa maisha yangu nani atakua ananisemea? …

Pampu Mpaka Maji Yatoke

Ukiwa kwenye kisima cha kupampu, ukipampu mara moja maji hayawezi kuja juu, ila ukipampu mara nyingi maji yatakuja juu. Na ukipampu na kuishia njiani bila kuona maji kama yale maji yalikuwa karibu kutoka yote yatarudi chini. Ukija kuanza tena utaanza upya. Katika maisha unapaswa kuwa na msimamo. Uwe na nguvu ya ung'ang'anizi. Kuwa na ung'ang'anizi …

Design a site like this with WordPress.com
Get started