Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hili Ndilo Sharti Namba Moja La Msamaha

Watu wanakosea namna ya kuombana msamaha hii inawasababisha watu kubaki na manung’uniko, chuki na hasira ndani ya mioyo yao.

Kusema naomba msamaha peke yake, bado hujamaliza kiu ya yule uliyemkosea. Kila anayeombwa msamaha kuna sauti ambayo anataka kuisikia kutoka kwa yule aliyemkosea.

Kwenye mahusiano yetu migogoro haiishi kwa sababu ya namna watu wanavyoombana msamaha. Mtu anaomba msamaha lakini bado anakuwa hajaondoa ule uchungu ulioumbika ndani ya moyo wake kwa sababu hajasikia ile sauti anayotaka kusikia ndani yake ili aachilie msamaha wa kweli.

Aina kubwa ya msamaha unaoendelea katika jamii zetu ni msamaha wa uongo. Watu wanasamehe kwa mdogo lakini bado wanakuwa na majeraha moyoni.

Sharti namba moja katika msamaha wa kweli ni mkosa kutambua kosa lake. Kwa mfano, umekosa usiishie tu kusema samahani basi kama nimekukosea.

Hivi kama hujamkosea mtu unaomba msamaha wa nini?
Pale unapokosa kwa mkosa au mkosewa wanapaswa kila mmoja kutambua kiini cha kosa na kukubali kosa.

Ukimkosea mtu kitu cha kwanza kiri kosa lako halafu ndiyo omba msamaha na hii ndiyo sauti ambayo watu wengi wanaokosewa wanataka kuisikia. Kwa mfano, samahani nimechelewa kufika kazini, naomba unisamehe. Kuliko tu kusema samahani basi kama nimechelewa kufika kazini.

Ukiwa mtu wa kukiri kosa lako, hata wale uliowakosea wanakusamehe kutoka ndani ya moyo kabisa kwa sababu wanaona kama umetambua kosa lako ya nini tena kuendelea kuwa na kisirani au kinyongo na wewe?

Watu ulio wakosea wanakuwa tayari kukusamehe endapo utakua mtu wa kukiri kosa kwa dhati na kutoka moyoni. Kwa mfano, katika harakati zako barabarani au sehemu yoyote ile unapishana na mtu na unamkanyaga mguuni, halafu unamwambia tu samahani. Ile samahani inakuwa bado haina nguvu kama ukimwambia samahani rafiki au ndugu nimekukanyaga bahati mbaya wala sikukusudia kufanya hivyo, kwahiyo, naomba unisamehe rafiki yangu.
Hapo mtu hata kama amekasirika utakua umeyeyusha hasira zake.

Hatua ya kuchukua leo;
Msamaha wa kweli unadai mhusika kutambua kosa lake, kabla hujaomba msamaha kwa yule uliyemkosea kiri kosa, tambua kosa lako na omba msamaha wa kweli.

Hivyo basi, kila wakati unapomkosea mtu tambua kuwa yule uliyemkosea anataka kusikia wewe ukikiri kosa lako na kulitambua.

Kwa mfano, kiimani tunasamehewa dhambi zetu kwa kukiri na kutubu. Ni ngumu kusamehewa kama aliyetenda kosa hajatambua kosa lake na kutubu.

Tusiwe tunafanya makosa halafu tunawaambia wenzetu kama Mungu anasamehe na wewe samehe pia.
Lazima upitie mchakato wa kutubu kwanza ndiyo upate ondoleo la dhambi.

Usiwe mbishi, kama umekosea kubali kosa lako na kisha omba msamaha wa kweli.

Muhimu;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504

https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: