Kila Ulichonacho Unaweza Kukipoteza Muda Wowote

Kila ulichonacho umekopeshwa. Kama unavyojua kitu cha kukopeshwa lazima ukirudishe kwa wenyewe pale wanapokihitaji. Vitu vyote ulivyonavyo, kuanzia watu wako wa karibu, mali, kazi, biashara nk umepewa kwa muda, itafikia wakati utavirudisha yaani utavipoteza. Na unatakiwa ujiandae pale vinapoondoka vile ulivyonavyo visikuumize. Jiambie kwamba, muda wake wa kuvirudisha umefika kwani niliazimwa kutumia kwa muda tu. …

Usishangae Kuona Mabadiliko Haya Hapa Kwenye Maisha Yako

Unapaswa kuelewa kwamba dunia haisimami. Na wewe pia hausimami, aidha hapo ulipo unaenda mbele au unarudi nyuma. Jichunguze, je, unaenda wapi? Kama dunia haisimami, basi unapaswa kujua kwamba kila kitu kinabadilika. Usishangazwe na mabadiliko unayoyaona kwa watu wengine. Watu wanabadilika na kila kitu kinabadilika. Watoto wanabadilika, ndugu, jamaa, marafiki na hata wenza wetu wanabadilika. Ishi …

Ili Uweze Kushinda Unahitaji Kupanga Kushinda, Karibu Ujifunze Namna Ya Kupanga Hapa

Je, unajua umezaliwa kushinda? Kila mtu anaweza kuwa mshindi kwenye maisha yake, kila mtu amezaliwa na uwezo mkubwa sana ndani yake. Lakini cha ajabu dunia imefanya kazi ya  kutuaminisha kwamba siyo kila mtu anaweza kufanikiwa, kitu ambacho siyo kweli. Kupitia kitabu hiki cha Kwanini Umezaliwa Kushinda utakwenda kupata majibu sahihi ya kwanini umezaliwa kushinda. Ufanye …

Kifahamu Kichocheo Cha Kufanya Au Kutokufanya

Pale unapofanya mambo mazuri unakuwa unajisikia vizuri wewe mwenyewe, na pale unapofanya mambo mabaya unakuwa unajisikia vibaya wewe mwenyewe. Kufanya au kutokufanya huwa kunachochewa na kitu kimoja ambacho ni msukumo wa ndani. Msukumo wa ndani ndiyo mchezo wa mambo yote yale. Hapa ndiyo injini ya sababu je, nifanye au nisifanye. Mtu anafanya kadiri ya msukumo …

Haya Ndiyo Maisha Mabaya Hapa Duniani, Epuka Kuwa Nayo

Maisha yasiyo na msimamo ni maisha mabaya yasiyoeleweka. Watu wengi wamekosa misimamo kwenye maisha yao. Hili ni kwenye kila eneo la maisha, watu wamepoteza msimamo. Na mtu asipokuwa na msimamo anapoteza ladha ya maisha kwa ujumla. Lazima uamue kuwa mtu wa msimamo. Ukiamua kufanikiwa kitu unakifanya kweli mpaka unaona matokeo mazuri. Wasiokuwa na msimamo huwa …

Jinsi Furaha Ya Kweli Inavyopatikana

Kila mtu anapenda awe na maisha ya furaha. Lakini furaha hizo zimekuwa hazidumu hata pale mtu anapopata furaha. Ni kama vile watu wanamkimbiza kipepeo, kila akikaribia kumkamata, kipepeo anakimbia. Wako watu wengine furaha yao iko kwenye vitu. Wanajitahidi kuwa na vitu vingi kadiri wa wezavyo ili tu wawe na furaha. Wanajitahidi kweli wanakuwa navyo lakini …

Epuka Hatua Hizi Za Kuchukua Linapokuja Suala La Mafanikio

Moja, epuka kutokuchukua hatua kabisa. Hapa mtu hafanyi kitu chochote kikubwa kwenye maisha yake. Mtu anajua anachotaka lakini hachukui hatua ya kuweza kukifikia na hivyo anaishia kushindwa kukipata. Mbili, kuchukua hatua kinyume. Yaani kukimbia. Hapa ni pale mtu badala ya kukabiliana na hali ngumu anayokutana nayo, ambayo kama akiivuka atafikia mafanikio makubwa, lakini yeye anaikimbia. …

Jinsi Ya Kuendelea Kumpenda Mwenza Wako Wa Ndoa

Wako ambao wamefikia hatua ya kuwachukia na kuwachoka wenza wao wa ndoa ili hali mwanzo walikuwa wanapendana kama kawaida. Kama mtu ataamua kumchukia mwenza wake wa ndoa maana yake atakua amevua upendo wa kweli na kuanza kujichukia yeye mwenyewe. Watu wanachokana mapema kwa sababu waliingia kwenye ndoa wakiwa na matarajio binafsi ambayo wangeyakuta  kutoka kwa …

Acha Njia Ya Matumaini Na Nenda Njia Hii

Binadamu tuhitaji matumaini na hata hamasa ili kutusukuma kuchukua hatua na kwenda mbele. Kuna changamoto moja ambayo nimeiona watu wengi wanajificha huko. Watu wengi wanajificha kwenye njia ya matumaini. Hapa mtu anakuwa hachukui hatua lakini anajipa matumaini makubwa lakini hana anachofanya kufikia matumaini aliyokuwa nayo. Watu wamekuwa na matumaini hewa tu ya kujifariji lakini hawaweki …

Usijilaumu Kama Ulifanya Hivi

Usipoielewa misingi ya dunia utapata shida sana. Huwa tunataka mambo yaende kama vile tunavyotaka sisi. Kifupi, dunia haiendi kadiri ya matakwa yetu. Bali,Dunia inajiendesha kwa misingi yake, inafanya inavyotaka na siyo vile tunavyotaka sisi. Maisha yetu sisi binadamu ni kama biashara. Kuna wakati unapata faida na kuna wakati unapata hasara. Kama unapata faida tu, jua …

Design a site like this with WordPress.com
Get started