Pale unapofanya mambo mazuri unakuwa unajisikia vizuri wewe mwenyewe, na pale unapofanya mambo mabaya unakuwa unajisikia vibaya wewe mwenyewe.
Kufanya au kutokufanya huwa kunachochewa na kitu kimoja ambacho ni msukumo wa ndani.
Msukumo wa ndani ndiyo mchezo wa mambo yote yale. Hapa ndiyo injini ya sababu je, nifanye au nisifanye.
Mtu anafanya kadiri ya msukumo wake wa ndani unavyomsukuma kufanya.
Kama mtu anataka kweli kufanya kitu, hakuna chochote cha nje kinachoweza kumzuia kufanya.
Na kama mtu hataki kabisa kufanya kitu, hakuna chochote cha nje kinachoweza kumlazimisha kufanya.
Mafanikio makubwa yanapatikana pale mtu anapokuwa na msukumo wa ndani.
Ukitaka kufanya kitu na mtu wewe angalia msukumo wake wa ndani ukoje, kama hana msukumo wa kufanya huko mbeleni mtasumbuana tu.
Mtu mwenye msukumo wa ndani huwa hakumbushwi nini anatakiwa kufanya bali anafanya kwa sababu anajua ni wajibu wake kufanya hivyo.
Tuwe watu tunaoongozwa na msukumo wa ndani katika kufanya mambo yetu na siyo vinginevyo.
Hatua ya kuchukua leo; ukitaka kufanya makubwa hakikisha unakuwa na msukumo wa ndani wa kufanya kitu hiko.
Msukumo wa ndani ndiyo utakupeleka kwenye mafanikio makubwa.
Kama mtu hasukumwi kufanya kutoka ndani wala usimsumbue achana naye maana mtasumbuana tu baadae.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog