Unapaswa kuelewa kwamba dunia haisimami. Na wewe pia hausimami, aidha hapo ulipo unaenda mbele au unarudi nyuma. Jichunguze, je, unaenda wapi?
Kama dunia haisimami, basi unapaswa kujua kwamba kila kitu kinabadilika.
Usishangazwe na mabadiliko unayoyaona kwa watu wengine.
Watu wanabadilika na kila kitu kinabadilika. Watoto wanabadilika, ndugu, jamaa, marafiki na hata wenza wetu wanabadilika.
Ishi kwa falsafa hii kwamba kila kitu kinabadilika, pale mambo yanapokwenda na usivyotarajia utajiambia nilijua tu kwamba kila kitu kitabadilika na hata hiki nilitarajia kitatokea.
Kwa matokeo mazuri au mabaya kwenye maisha yako yasikushangaze kabisa kwani kwenye maisha lolote linaweza kutokea.
Ukiona watu walikuwa na tabia fulani na sasa wamekuwa na tabia ambayo wewe mwenyewe hupendezwi nayo, usishangazwe na mabadiliko hayo, kwani ni kawaida ya watu kubadilika.
Huwezi kuzuia watu au vitu visibadilike kwani ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako.
Hatua ya kuchukua leo; usishangazwe pale vitu au watu wanapobadilika ni kanuni ya asili watu kubadili na tegemea hilo kila wakati na jikumbushe kuwa watu kubadilika ni sehemu tu ya maisha.
Kwahiyo, elewa kwamba kwenye asili kila kitu kinabadilika na hakuna chochote kitabaki kama kilivyokuwa.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog