Wako ambao wamefikia hatua ya kuwachukia na kuwachoka wenza wao wa ndoa ili hali mwanzo walikuwa wanapendana kama kawaida.
Kama mtu ataamua kumchukia mwenza wake wa ndoa maana yake atakua amevua upendo wa kweli na kuanza kujichukia yeye mwenyewe.
Watu wanachokana mapema kwa sababu waliingia kwenye ndoa wakiwa na matarajio binafsi ambayo wangeyakuta kutoka kwa wenza wao sasa pale mtu anapoingia na kukosa kile akichokuwa anakitarajia ndiyo matatizo huanzia hapo.
Iko njia ambayo itakusaidia kuepuka kumchoka au kumchukia mwenza wako ambayo ni kumchukulia mwenza wako kama wanafunzi na wewe ukiwa ndiyo mwalimu wake.
Kikawaida, mwalimu yeyote yule mwenye moyo wa kufundisha kweli hawezi kumchukia mwanafunzi wake ambaye hajui kitu fulani. Bali atajitahidi kweli kuhakikisha anampambania mwanafunzi wake aweze kuelewa na kuwa bora na hatimaye afaulu kwenye mtihani na maisha kiujumla.
Hata wewe tumia mbinu hii, muone mwenzako ni kama mwanafunzi hivyo unatakiwa kumfundisha kwa upendo ili aweze kubadilika.
Na mwanafunzi hawezi kuwa bora siku moja, kila siku ni kazi ya kumfanya awe bora.
Mwenza wako awe ni mwanafunzi wako wa maisha yako yote ya hapa duniani mpaka pale kifo kitakapowatenganisha.
Uwe mwalimu mzuri kwa mwenza wako, mfundishe vizuri kwa upendo na kila siku weka jitahidi za kumfanya kuwa bora.
Ni ujinga pale unapomwona mwenza wako hajui kitu fulani ndiyo iwe fimbo ya kumchapia. Ona kwamba mwenza wako asipokuwa anajua kitu wewe mwalimu wake ndiyo una makosa, mfundishe kama unataka awe bora.
Safari ya ndoa ni ya kuvumiliana na kusikilizana. Wewe ukiwa kama mwalimu wa mwenza wako mvumilie na msikilize mwanafunzi wako pale unapokuwa unamfundisha.
Huwezi kumpata mtu aliyekamilika kwa kila kitu. Cha msingi ni wewe kubaki njia kuu, endelea kunywa maji ya kisima chako mwenyewe.
Kama maji ya kisima chako yamechafuka safisha kisima chako ili uendelee kupata maji masafi na kuachana na kukimbilia visima vya watu.
Hatua ya kuchukua leo; mchukulie mwenza wako wa ndoa, kama mwanafunzi wako wa maisha yako kwa kipindi ambacho uko naye hapa duniani.
Kuwa mwalimu mzuri kwa mke au mume wako, hakikisha unamfundisha na kuwa bora kama vile anavyotaka. Pale unapoona anashindwa kufaulu, jua basi somo halijaeleweka vizuri, rudia tena mpaka upate matokeo mazuri unayotaka kuyaona kwa mwenza wako wa ndoa.
Ili kuendelea kunogesha mahusiano yako kiujumla nakusihi sana usome kitabu cha Ijue Njaa Ya Wanandoa, kitabu hiki ni shilingi elfu 15 tu, ambacho kipo katika mfumo wa nakala ngumu. Pata kitabu hiki leo ili uyafanye maisha yako ya ndoa kuwa ya furaha na siyo kuvumilia. Kupata kitabu chako piga namba 0717101505 au 0767101504
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog