Samaki Huwa Anaanza Kuozea Kichwani

Ukiwa na tatizo lolote lile katika uongozi wako basi jua wewe ndiyo tatizo. Wasaidizi wako hawawezi kuwahi kazini kama wewe unachelewa. Unapokuwa kiongozi watu wanafanya vile ambavyo wewe unafanya. Ukiwa ni mtu wa kuwajibika basi na wale unaowaongoza watawajibika. Ndiyo maana nimeanza na kusema samaki huwa anaanza kuozea kichwani. Yaani mambo yakiharibika mhusika mkuu ni …

Kitabu Kipya; Jinsi Ya Kutengeneza Bahati Yako

Mpendwa rafiki yangu, Kwa furaha kubwa napenda kutumia nafasi hii kukujulisha kuwa nimezindua kitabu kipya kiitwacho Jinsi Ya Kutengeneza Bahati Yako. Natumaini nilishakueleza ndoto yangu ya kuandika vitabu 100 mpaka ifikapo tarehe 30/9/2030 na kitabu cha leo ni mchakato wa kufikia vitabu hivyo 100. Na ni kitabu cha jinsi ya kutengeneza bahati yako kweli, mimi …

Uza Vitu Ambavyo Mteja Anavihitaji

Siku zote soko huwa halina huruma na mtu. Huwa linafanya vile linavyotaka lenyewe. Ukitaka kuuza chochote kile lazima ujue soko linataka nini. Na mara nyingi yule anayeuza ni yule anayejua soko linataka nini, unaweza ukajipanga kuingia sokoni na bidhaa zako lakini usiuze yote ni kwa sababu hujacheza na soko. Uza vitu ambavyo mteja anavihitaji kweli. …

Biashara Ni Kama Maigizo

Ili uweze kuuza kwenye biashara yoyote ile unapaswa kukaa upande wa mteja mara zote. Ukiwa kinyume na mteja mara nyingi huwa anaondoka na kwenda kwa yule ambaye ana mjali na yuko upande wake. Hata kama unaona mteja hayuko sahihi siyo kazi yako wewe kumrekebisha wewe kazi yako ni kuuza na kupata faida. Ukishakuwa kwenye biashara …

Chukua Hatua Bila Kuambiwa

Siku moja nilikuwa safarini nikakutana na rafiki ambaye tulikaa siti moja kwenye basi. Katika maongezi mengi tuliyoongea akanisimulia hadithi ya kweli ambayo inamhusu yeye mwenyewe. Anasema siku moja alienda kupata chakula kwenye moja ya mgahawa. Mmoja wa wateja alienda kunawa mikono na kuacha bomba la maji likiwa linatiririka. Yeye aliacha kula akaenda kufunga yale maji …

Aina Mbili Za Ujasiri Unazopaswa Kuwa Nazo Ili Ufanikiwe

Wengi wanatamani kuwa na mafanikio lakini cha ajabu hawana ujasiri wa kufikia ndoto zao. Bila kuwa na ujasiri ni ngumu sana kufanikiwa. Ujasiri ni kuweza kutenda licha ya kuwa na hofu. Ujasiri siyo kutokuwepo kwa woga. Kiasili kila binadamu huwa na hofu na woga pale anapotaka kufanya jambo jipya, sasa kitendo cha kuthubutu bila kujali …

Ubaya Au Uzuri Wa Kitu Unatokana Na Kitu Hiki

Unatokana na tafsiri yako. Kiasi asili hakuna kitu kibaya wala kizuri. Ubaya au uzuri ni zile tafsiri ambazo sisi wenyewe tunazitoa juu ya kitu fulani. Vitu huwa vinatokea kwa namna vinavyotokea na uzuri au ubaya wa kitu ni tafsiri yako ndiyo inatoa. Kitu kinachowaumiza watu siyo kile kinachotokea ila jinsi watu wanavyotafsiri kile kinachotokea. Kwa …

Kuwa Na Viwango Vyako Kwenye Kila Eneo La Maisha

Kujilinganisha na wengine ni kitu kigumu kufanya. Badala ya kujilinganisha unapaswa kuwa na viwango vyako ili utembee navyo kwenye safari ya mafanikio. Haijalishi unafanya nini kwenye maisha, kuna mtu ambaye ni bora kuliko wewe, ukikazana ukawa na baiskeli, kuna mwenye pikipiki, ukiwa na pikipiki kuna wenye magari na ukiwa na gari kuna wenye ndege. Hivyo …

Dalili Za Kuanza Kufa

Ni kanuni ya maisha kwamba chochote ambacho hakikui basi kinakufa. Kwa mfano, kama haukui kwenye kazi yako, kila siku uko vile vile unafanya kwa mazoea ni dalili ya kuanza kufa kwenye eneo hilo. Hata kwenye biashara, kama haiendelei kukua kadiri ya muda unavyokwenda inakuwa inakufa. Katika mahusiano, mahusiano ambayo hayakui iwe ni ndoa au mahusiano …

Design a site like this with WordPress.com
Get started