Design a site like this with WordPress.com
Get started

Chukua Hatua Bila Kuambiwa

Siku moja nilikuwa safarini nikakutana na rafiki ambaye tulikaa siti moja kwenye basi. Katika maongezi mengi tuliyoongea akanisimulia hadithi ya kweli ambayo inamhusu yeye mwenyewe.

Anasema siku moja alienda kupata chakula kwenye moja ya mgahawa. Mmoja wa wateja alienda kunawa mikono na kuacha bomba la maji likiwa linatiririka.

Yeye aliacha kula akaenda kufunga yale maji ili yasiendelee kutoka.

Wakati anaenda kulipia bili, mmiliki wa huyo mgahawa akamwambia usilipe bili, bili yako tayari nimeshakulipia.

Akamuuliza kwa nini? Akamwambia nimekulipia kwa sababu ya kujitoa kwako kwenda kufunga maji yaliyokuwa yanamwagika huku wengine wakiwa hawajali.

Akamwambia umenisaidia sana kupunguza gharama na kama watu wote wangekuwa kama wewe dunia ingekuwa bora sana.

Hapa tunapata funzo gani?

Tunajifunza kuwa unapaswa kujituma bila kuambiwa.

Kujituma bila kuambiwa inakusaidia kuongeza thamani na hatimaye kujitengenezea bahati.

Jali vitu vya watu wengine kama vile ni vyako.

Jambo lolote lile unaloona haliko sawa na liko ndani ya uwezo wako lifanyie kazi mara moja siyo mpaka uambiwe.

Jitume kuchukua hatua pale unapoona mambo hayako sawa.

Usiwe mtu wa kusubiri kuambiwa hata siku moja. Jitume wewe mwenyewe kwanza kabla hujawatuma wengine.

Juhudi binafsi zitakusaidia kufanikiwa na kujitofautisha na wengine.

Hatua ya kuchukua leo; chochote kile ambacho hakipo sawa na kipo ndani ya uwezo wako kukirekebisha, basi kirekebishe mara moja.

Mwisho, chukua hatua bila kuambiwa, usisubiri upigiwe kengele, angalia kama kitu hakipo sawa, basi kiweke sawa na kama kitu siyo kweli na watu wanasimamia kwenye uongo wewe simamia kwenye ukweli.

Utakatifu haupatikani kwa njia ya kusali tu, bali unapatikana kufanya mambo madogo ambayo tuko nayo kila siku.

Kumbuka nyota yako iko kwenye kile unachofanya, utang’ara kwa kufanya vizuri na kwa uaminifu mkubwa.
Fanya kazi yako vizuri na dunia itanufaika na wewe kwa namna unavyotenda mambo yako.

Ng’ara pale ulipopanda yaani bloom where you’re planted

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: