Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ubaya Au Uzuri Wa Kitu Unatokana Na Kitu Hiki

Unatokana na tafsiri yako.

Kiasi asili hakuna kitu kibaya wala kizuri. Ubaya au uzuri ni zile tafsiri ambazo sisi wenyewe tunazitoa juu ya kitu fulani.

Vitu huwa vinatokea kwa namna vinavyotokea na uzuri au ubaya wa kitu ni tafsiri yako ndiyo inatoa.

Kitu kinachowaumiza watu siyo kile kinachotokea ila jinsi watu wanavyotafsiri kile kinachotokea. Kwa mfano, matokeo ya kitu yanapotokea huwa kiasili hayana shida ila sasa binadamu huwa tunaanza kuyachambua matokeo hayo kadiri ya tafsiri zetu.

Tafsiri yako ndiyo inaamua uzuri au ubaya wa kitu.

Zile kwanini unazojiuliza ndiyo zinapelekea kuona kitu kibaya au kizuri. Mtazamo wako ndiyo chagua lako.

Kinachowaumiza watu siyo tukio lililotokea bali tafsiri wanayoitoa juu ya lile tukio lililotokea.

Kuwa makini na maana unazozitengeneza juu ya kitu fulani kwani hizo ndiyo zinakufanya uumie. Acha mambo yatokee kama yalivyopangwa kutokea, kwa mfano, mwingine anapata shida kwanini mvua hazinyeshi au jua linawaka sana, hivi ni vitu ambavyo vinajiendesha kadiri ya asili na siyo matakwa yetu.

Jua kwamba chochote kile kinachotokea kwenye maisha yako kuna funzo ndani yake. Kwenye kila baya kuna zuri ndani yake.

Hatua ya kuchukua leo; chochote unachojiambia hiyo ni tafsiri yako unaweza kuibadili vile unavyotaka.

Kinachokufanya upate maumivu ni zile tafsiri unazoumba juu ya kile kinachotokea.

Vione vitu kama vilivyo na acha kuviumba kwa tafsiri yako binafsi. Ukiona kitu kinakuumiza au kinakufurahisha jua kabisa hiyo maana umeitengeneza wewe mwenyewe.

Unao uamuzi wa kutengeneza maana chanya au hasi. Kazi ni kwako, usijitese kwa maana unazotengeneza juu ya kitu fulani, amini kwamba vitu huwa vinatokea kwa namna vinavyotokea kadiri ya tafsiri yako mwenyewe.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: