Design a site like this with WordPress.com
Get started

Biashara Ni Kama Maigizo

Ili uweze kuuza kwenye biashara yoyote ile unapaswa kukaa upande wa mteja mara zote.

Ukiwa kinyume na mteja mara nyingi huwa anaondoka na kwenda kwa yule ambaye ana mjali na yuko upande wake.

Hata kama unaona mteja hayuko sahihi siyo kazi yako wewe kumrekebisha wewe kazi yako ni kuuza na kupata faida.

Ukishakuwa kwenye biashara mara zote kuwa upande wa mteja wako, vitu kama imani, siasa, ushabiki au hisia anavyoamini mteja kubaliana naye na wala usitake kumkosoa mwache aamini kile anachokiamini yeye.

Wewe kama muuzaji unapaswa usiwe upande wowote ule, hata kama una ushabiki wa kitu fulani, iwe ni siri yako usimwoneshe mteja wako. Ila kuwa upande wake kwa kile anachokiamini yeye.

Kocha Dr Makirita Amani anasema biashara ni kama maigizo, igiza uwezavyo ili uweze kufanya mauzo.

Kwa kuwa kila mmoja wetu ni muuzaji basi anapaswa kufanya maigizo awezavyo ili aweze kufanya mauzo kwenye eneo analotaka mauzo mazuri.

Unahitaji mauzo mazuri kwenye biashara, ndoa, mahusiano kiujumla nk. Kuna wakati mahusiano yanakuwa magumu kwa sababu wahusika hawafanyi maigizo ili waweze kuuza.

Kufanya maigizo ni kumpatia mteja kile anachotaka kutoka kwako. Kufanya maigizo ni kutimiza matarajio ya mteja.

Kila mmoja wetu anapenda kuthaminiwa na anatarajia akiingia sehemu fulani atapata kitu fulani hivyo anapokuja kwako na akakikuta hapo utakua umemweza na akija kwako akikosa kile alichokuwa anatarajia lazima atakakwazika na kutafuta sehemu nyingine anayoweza kupata kile anachotaka.

Hatua ya kuchukua leo; Kila unayehusiana naye ni mteja wako hakikisha kile ambacho mteja wako anatarajia kukipata kutoka kwako kwa njia ya biashara, ndoa, kazi, urafiki nk anakipata.

Mara nyingi vitu vingi vinavyotuzunguka huwa vinakufa kwa sababu ya kukosa mauzo. Mauzo ndiyo uhai wa kitu chochote kile ambacho kinafanya uhai wa kitu hiko uendelee kuwepo.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: