Siku zote soko huwa halina huruma na mtu. Huwa linafanya vile linavyotaka lenyewe.
Ukitaka kuuza chochote kile lazima ujue soko linataka nini.
Na mara nyingi yule anayeuza ni yule anayejua soko linataka nini, unaweza ukajipanga kuingia sokoni na bidhaa zako lakini usiuze yote ni kwa sababu hujacheza na soko.
Uza vitu ambavyo mteja anavihitaji kweli. Uza vitu ambavyo soko linahitaji kweli.
Wakati mwingine hupaswi kuuza kitu kwa matakwa yako, uza kadiri soko linavyotaka.
Rahisisha mteja apate huduma kwa haraka na wakati. Kama wateja wa sasa wanahitaji uharaka na hawana muda wa kusubiri na wewe ukiwa unawachelewesha ni wazi kabisa watakukimbia.
Soko ndiyo huwa linaamua, hivyo uza kadiri soko linavyotaka na siyo wewe unavyotaka.
Hatua ya kuchukua leo; jitathimini je, vile unavyouza soko au wateja wanavihitaji kweli?
Kwahiyo, ili upate ushindi kwenye soko au kwa mteja uza vitu ambavyo mteja anavihitaji.
Wakati mwingine una bidhaa lakini huna unachouza, hapo huenda shida ikawa unaenda kinyume na soko.
Jua soko linataka nini yaani watu halafu wape kile wanachotaka. Ulishawahi kujiuliza nani anapanga bei ya maembe sokoni?
Soko ndiyo huwa linaamua bei ya bidhaa yoyote ile sokoni.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog