Maisha ni mauzo na yeyote anayeweza kuuza vizuri zaidi ndiye anayefanikiwa.
Na utaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako kama utaweza kuuza zaidi.
Tunauza muda wetu, utaalamu wetu, uzoefu wetu, huduma zetu na hata bidhaa mbalimbali.
Pia tunauza mawazo yetu, ushawishi wetu na hata ndoto na maono makubwa tuliyonayo.
Mauzo huwa hayaishii pale tu mteja anaponunua, bali ndiyo yanaanza.
Mteja akishanunua, jua imani yake kwako ni kubwa, hivyo angalia kipi zaidi unaweza kumuuzia na atakuwa tayari kununua zaidi na zaidi, kama ulichomuuzia mwanzo ni sahihi kwake.
Hatua ya kuchukua leo; endelea kumfuatilia mteja aliyenunua kwako ili aendelee kununua.
Kumbuka , mauzo hayana mwisho bali ndiyo kwanza yanaanza pale tu unapofanikiwa kumuuzia mteja.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog