Huwa anafanya na anakipata. Ikiwa mtu hataki kitu, hawezi kukuambia ukweli bali atakuonesha sababu ambazo ukizichunguza vizuri unakuta siyo za kweli ila anakupa sababu kwa sababu anaogopa kukuambia ukweli na akikuambia ukweli utajisikia vibaya. Mtu ambaye anataka kitu utaona nia yake ya kweli hata kama amewekewa vipingamizi. kwa mfano, watu watano waliitwa katika usaili, watatu …
Kama Unataka Kuwa Bora
Jitahidi kufanyia kazi kwa vitendo yale yote unayajua kadiri ya vile unavyotaka kuwa bora kupitia kile unachofanya. Unajua kwamba kuamka mapema, inaleta afya, utajiri na hekima basi amka mapema na fanya hivyo utaona matokeo. Usitamani mafanikio ambayo hujayakalia katika mchakato. Kama unataka kuwa muuzaji bora kuwahi kutokea, jitahidi kufanya mazoezi ya mauzo na kujifunza kila …
Kila Siku Tafuta Mteja Mpya
Kwenye biashara yoyote ile unayofanya au unayotarajia kufanya kamwe usitegemee mteja mmoja. Kila siku kwako iwe ni siku ya kutafuta wateja wapya kwa sababu wateja ulionao wako ambao wataacha kununua kwako na kununua kwa mtu mwingine. Wateja wanahama, wanabadilika, wanakufa nk hivyo ili UJIHAKIKISHIE ushindi ,mara zote kaa kwenye mchakato wa kutafuta wateja wapya. Kutegemea …
Nidhamu Ambayo Wengi Hawana
Ni nidhamu binafsi ya kujifuatilia. Ni rahisi mtu kufuatilia jinsi dunia inavyoenda kwenye mitandao ya kijamii, vyombo vya habari nk lakini wanajisahau kujifuatilia wao wenyewe. Kujifuatilia ni kazi, inahitaji nidhamu kali na wengi hawana, mtu anaweza kufuatilia Mambo ya wengine wakati hata kwake mwenyewe ameshindwa hata kufuatilia maendeleo ya watoto wake. Fuatilia namba muhimu kwenye …
Nyumba Usiyolala Hujui Hila Yake
Ukiwa nyumbani kwako ukiziangalia nyasi za jirani yako kwa mbali unaona za kijani kweli, unavutiwa nazo na kuziona za kwako siyo za kijani kama za jirani yako, ila ukizisogelea karibu unaona siyo za kijani kama ulivyoziona na ukiziangalia za kwako wakati uko kwa jirani unaona tena nyasi zako ni nzuri. Hapa tunapata somo gani? Tunapata …
Funga Hiyo Biashara
Kama una biashara na una msaidizi au wasaidizi ambao wanakusumbua lakini unashindwa kuwafukuza, funga hiyo biashara. Ukiona mtoto au msaidizi wako anakupanda kichwani hataki kutii mamlaka basi hapo jua huna mtoto wala msaidizi. Kama mmiliki wa biashara unatakiwa kua na maamuzi magumu dhidi ya biashara yako. Umeajiri ndugu au watu wako wa karibu halafu wanafanya …
Bila Maumivu Mteja Hawezi Kununua
Siyo tu bila maumivu mteja hawezi kununua bali pia bila maumivu huwezi kuuza. Maumivu aliyonayo mtu ndiyo yanamsukuma kuchukua hatua katika mauzo. Kama mtu hana maumivu hakuna chochote kitakachomshawishi kuchukua hatua kwa mfano, wewe unauza dawa ya kufunga kuharisha na mteja anakuja kwako akiwa anaumwa sana, na wewe umeshajua maumivu ya mteja ni kupata dawa …
Kuwa Polisi Wa Muda Wako
Akitokea mtu anakunyang'anya laki moja yako hutakubali kirahisi, utapambana mpaka dakika ya mwisho. Lakini ikitokea mtu anatumia muda wako vile anavyotaka wala huna wasiwasi utamchekea tu. Watu wanasahau sana thamani ya muda wao kwamba muda ndiyo unawaletea fedha. Kwa mfano, kama thamani ya muda wako kwa saa ni laki moja hivyo kila dakika moja utakua …
Una Maoni Kila Mahali Lakini Huna Maoni Juu Yako
Unatoa maoni kwenye michezo mbalimbali inayoendelea duniani. Unatoa maoni kwenye maisha ya watu wanavyoishi. Unatoa maoni kwenye siasa na nchi kwa ujumla inavyoenda. Kifupi unatoa maoni kila mahali lakini hutoi maoni kwenye maisha yako binafsi. Ukiacha kutoa maoni kwenye kila kitu na kutunza muda huo kwenye kufanya kazi, na kujitathimini binafsi, kwa nini uko hivyo …
Continue reading "Una Maoni Kila Mahali Lakini Huna Maoni Juu Yako"
Kama Huna Shauku Unakuwa Umekosa Hiki
Shauku ndiyo sifa inayolipa duniani kuliko sifa zote. Kwa chochote kile unachokwenda kukifanya leo, nenda kakifanye kwa shauku na utajenga ushawishi lakini pia kukubalika na kufanikiwa kwenye kile utakachofanya. Mtu ambaye hana shauku anakuwa amekosa ladha. Anakuwa kama chakula kilichokosa chumvi kinakosa ladha. Pata picha unajisikiaje ukila chakula ambacho hakina ladha? Kinakuwaje? Unapokuwa unafanya chochote …