Kwenye biashara yoyote ile unayofanya au unayotarajia kufanya kamwe usitegemee mteja mmoja.
Kila siku kwako iwe ni siku ya kutafuta wateja wapya kwa sababu wateja ulionao wako ambao wataacha kununua kwako na kununua kwa mtu mwingine.
Wateja wanahama, wanabadilika, wanakufa nk hivyo ili UJIHAKIKISHIE ushindi ,mara zote kaa kwenye mchakato wa kutafuta wateja wapya.
Kutegemea wateja wachache ni kujiandaa kushindwa kwenye mauzo.
Kuwa na wateja wachache ni hatari kwa sababu watakuja kuathiri mauzo yako.
Kwa sababu mauzo ni moyo wa biashara hivyo kila siku tafuta wateja wapya ambao watanunua hata wale unaowategemea wasiponunua hawatakuathiri.
Hatua ya kuchukua leo; usitegemee mteja mmoja, kila siku tafuta mpya.
Kuwa na wateja wengi ni utajiri mzuri kwenye biashara au huduma unayotoa. Jitahidi kujisukuma ili uwe wateja wapya kila siku.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog