Siyo tu bila maumivu mteja hawezi kununua bali pia bila maumivu huwezi kuuza.
Maumivu aliyonayo mtu ndiyo yanamsukuma kuchukua hatua katika mauzo.
Kama mtu hana maumivu hakuna chochote kitakachomshawishi kuchukua hatua kwa mfano, wewe unauza dawa ya kufunga kuharisha na mteja anakuja kwako akiwa anaumwa sana, na wewe umeshajua maumivu ya mteja ni kupata dawa ili afunge kuharisha hapo ni rahisi kumshawishi kununua.
Shabaha yangu ni kutaka kukuambia kuwa unapoouza kitu ili mtu anunue hakikisha kwanza umetengeneza mazingira ya tamaa na maumivu ambayo yatamsukuma mteja kununua kile unachouza.
Na maumivu ni kile ambacho kinamsukuma mteja kuchukua hatua. Wewe unauza kifaa cha kuogelea na unakutana na mtu ambaye baharini anazama kwa sababu hana kifaa cha kuogelea mtu huyo tayari ana maumivu hata hitaji tena bei anachotaka yeye umpatie kifaa ili aweze kuokoa uhai wake.
Hatua ya kuchukua leo; hakikisha unajua maumivu ya mteja wako, jua kile ambacho kinamsukuma mteja kuchukua hatua.
Unaweza kujiona kama vile una kisirani, kwa sababu huuzi, unachotakiwa kufanya ni kujua maumivu ya wateja wako na utaweza kuuza.
Mauzo ni mchakato, jua kile kinachowaumiza watu kisha wasaidie kukipata na utaweza kuuza.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog