Utumwa Pekee Unaopaswa Kuwa Nao

Kuliko kuwa mtumwa wa kulalamika, kukata tamaa na kila aina ya mtazamo hasi.Wewe kuwa mtumwa wa MATUMAINI Kuwa mtumwa wa MATUMAINI, amini katika ndoto zako, amini mambo yanawezekana na endelea kukaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachoamini. Kuwa mtumwa wa MATUMAINI lakini hakikisha uko katika mchakato sahihi. Usiwe na matumaini kama hauko katika njia sahihi. …

Fanya Kama Vile Hutaki Pesa

Kuna kitu kimoja cha kushangaza kwenye tabia za binadamu, watu huwa wanahangaika na kile ambacho hakiwajali. Kwa mfano, Benki huwa zinawapa mikopo wale ambao hawazihitaji sana hizo fedha za mikopo. Makampuni makubwa ya sanaa huwa yanawapa mkataba wasanii ambao hawahitaji hata mkataba wao.Watu huwa wanawapenda sana watu ambao hawana hata muda nao. Ni kanuni ya …

Nafasi Za Kazi

Watu wanalalamika kuwa hakuna nafasi za kazi. Lakini siyo kweli, nafasi za kazi zipo ila changamoto ni watu.Waajiri wengi wanakuwa na maono makubwa lakini wanakosa watu sahihi wakusaidiana nao. Utakuja kuliona hili changamoto siyo kazi, bali changamoto ni watu. Nafasi za kazi zipo ila changamoto ni watu.Watu ni rahisi kuanzisha kitu lakini ni wagumu kumaliza …

Kama Kweli Unampenda Wa Kwanza, Usingefanya Hivi

Mtu mmoja aliwahi kusema, kama umewapenda watu wawili na unatakiwa kubaki na mmoja, unatakiwa kumchagua wa pili. Kwa sababu kama ungekuwa unampenda kweli wa kwanza usingeenda kwa wapili.Hapa tunajifunza nini? Kile ambacho unakipa muda sana kwenye maisha yako ndiyo unakipenda. Hivyo basi, unatakiwa kukipa muda kitu ambacho unakipenda ili kiweze kukupa matokeo mazuri.Biashara na kazi …

Huwezi Kujikimbia

UENDAPO NDIPO ULIPO, HUWEZI KUJIKIMBIA.Watu wengi wanapokuwa na msongo au sonona, huwa wanaona kubadili mazingira kwa kusafiri itabadili hali yao.Lakini hilo siyo linalotokea, pamoja na kusafiri, watu bado hujikuta wakiendelea kuwa kwenye hali zile zile. Sasa Mwanafalsafa Seneca anatufundisha kwamba kitakachobadili hali zetu siyo kubadili mazingira yetu, bali kubadili mtazamo na fikra zetu.Kama hutabadili mtazamo …

Punje Ya Mhindi

Punje ya mhindi,Ina nguvu kubwa sana kama ikiwekwa katika mazingira sahihi. Ukikaa nayo ndani itabaki kama ilivyo. Lakini punje ya mhindi ukiiweka katika ardhi itakuletea maajabu. Hapa tunajifunza nini? Chochote kile kama ukikitumia vizuri lazima kikuletee matokeo. Na chochote kile kama ukitumia ndivyo sivyo lazima kikuletee matokeo ambayo siyo sahihi. Tunajifunza kwamba, ndani yetu kuna …

Usikubali Majuto Haya Yakukute

Kwenye maisha kuna majuto ya aina mbili, Moja majuto ya kufanya kitu. Mbili, majuto ya kutokufanya kitu. Majuto mabaya sana ni majuto ya kutokufanya. Ni bora ufanye hata baadaye mambo yakienda tofauti basi utasema KWELI, nimeshindwa lakini nimefanya.Kazi yako wewe ni kufanya. Kazi yako wewe ni kujaribu. Kazi yako wewe ni kushusha nyavu chini. Kwa …

Jinsi Ya Kupiga Hatua Mpya

Kwenye jambo lolote lile, huwa tunajenga tabia na kisha tabia zinatujenga. Na ili tupige hatua mpya lazima tujenge kwanza tabia mpya. Bila tabia mpya hakuna hatua mpya. Swali la kujiuliza, tabia ulizonazo sasa zinaendana na hatua unazopiga? Ukiona tabia na hatua unazopiga haziendani, unachotakiwa kufanya ni kujenga tabia mpya na hatua mpya. Unaweza kufanya kitu …

Ukishindwa Kufanya Kitu Ambacho Kipo ndani Ya Uwezo Wako

Ukishindwa kufanya kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako huo ni uvivu na uzembe.Watu huwa hawapendi kuambiwa maneno makali kama vile wewe ni mvivu au mzembe. Kama hupendi kuambiwa hayo maneno basi fanya kazi na kuwa makini.Pale unapojikuta katika hali ya kutokufanya kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako jikamate mwenyewe na jiambie kwamba wewe …

Design a site like this with WordPress.com
Get started