Tunayafanya maisha yetu kuwa magumu kwa sababu ya kuhangaika na vitu vipya kila siku. Tuliyokuwa nayo, bado hatujaweza kuyafanya vizuri kiasi kwamba tuende tukahangaike na vitu vipya. Hii inakuwa kama akili za mkulima kichaa. Mkulima kichaa ni yule ambaye anapanda mbegu leo kesho anaenda kufukua na kuangalia kama imeota. Kama haijaota anaenda tena kupanda sehemu …
Mambo Ni Yale Yale
Ndiyo, mambo ni yale yale lakini kinacholeta utofauti ni ufanyaji.Wako ambao wanafanya kwa kawaida na wanapata matokeo ya kawaida.Na wako ambao wanafanya kwa utofauti na kupata matokeo mazuri zaidi. Vyombo unavyotumia nyumbani siyo vipya kila siku. Ni vile vile, vinatumika, vinaoshwa na hivyo ndivyo ilivyo kwenye kukaa kwenye mchakato. Mambo ni yale yale. Unaweza kuona …
Mradi Mkuu Wa Biashara Yako
Kama unafanya biashara na wewe ndiyo mmiliki wa biashara hiyo, wewe ndiyo mradi mkuu kwenye biashara yako. Ili biashara yako ikue, unapaswa kujifunza zaidi. Achana na mazoea, na kila siku weka kazi ya kujifunza ili kuwa bora sana.Kama wewe ndiyo mradi mkuu kwenye biashara yako, unapaswa kuwa kioo kwa wengine wanaokuangalia. Unapaswa kuijua biashara yako …
Njaa Inayowasumbua Watu Wengi Zama Hizi
Tunaishi kwenye zama ambazo hazina utulivu wa akili. Kwa sababu, watu wako bize na mitando ya kijamii inawafanya watu kushindwa kuwajibika vizuri kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yao. Kutokana na ubize ambao watu wanakuwa wanao, wanakuwa wanatengeneza njaa kwenye maeneo mengine ya maisha yao. Njaa inayowasumbua watu wengi zama hizi, ni njaa ya kusikilizwa. Tukianza …
Kitu Ambacho Watu Wengi Hawana
Watu wengi wamekosa kitu kinachoitwa ustaarabu. Watu wengi hawana ustaarabu ndiyo maana mtu anaweza kumfanyia mwingine kitu ambacho siyo sahihi. Kama mtu una ustaarabu, huwezi kufanya kitu ambacho siyo sahihi. Kukosekana kwa ustaarabu kwenye jamii, hupelekea watu kuwa na maisha ya hovyo. Jamii imekuwa siyo ya kuaminika na watu wamekuwa ni janja janja. Watu hawana …
Jambo La Msingi Kwenye Maisha Yako
Fanya vitu vyote lakini usiache kufanya vitu vya msingi kwenye maisha yako. Na kupambania lengo lako ndiyo jambo la msingi. Fanya uwezavyo lakini usiache kupambania lengo. Drama ni nyingi kwenye maisha. Kiki ni nyingi ambazo zinakukwamisha wewe kutokufikia kwenye malengo yako. Puuza vitu vyote lakini usipuuze kupambania lengo lako kuu.Kila unapoamka asubuhi, jikumbushe lengo lako …
Unajizima Data
Kujizima data ni pale ambapo unakuwa unaambiwa kitu au kupata maelekezo ya kitu fulani halafu unafanya tofauti na maelekezo uliyopewa. Unakuwa unajua unachopaswa kufanya lakini unajifanya kama hujui kwa kufanya kile ambacho siyo sahihi. Kama vile unapima hebu tuone itakuwaje kama nisipofanya hivi. Unakuwa unamjaribu mhusika je atasemaje? Mtu makini na kazi yake au yule …
Usiende Safari Ndefu Ukiwa Huna Mafuta Yakutosha
Dereva yoyote anayetaka kusafiri safari ndefu lazima lazima atahakikisha gari lake liko vizuri. Na kitu muhimu zaidi ni kuangalia kama mafuta yako ya kutosha. Kwa sababu, asije akaanza safari halafu katikati ya safari mafuta yameisha na kushindwa kuendelea na safari. Katika mafanikio makubwa, ni safari ya ndefu. Ni safari ambayo inahitaji uwe unajaza mafuta mara …
Continue reading "Usiende Safari Ndefu Ukiwa Huna Mafuta Yakutosha"
Unatakiwa Ufikie Kiwango Hiki
Kwenye maisha unatakiwa kujijengea sifa ambayo mtu anakuwa hana shaka yoyote ile juu yako. Kwa mfano, mtu akikuachia kazi, asiwe na wasiwasi aende akalale hata usingizi. Tunataka mtu akikupa kazi na anaenda kulala. Yaani mpe mtu kazi na ukalale usingizi. Je, umefikia viwango hivyo? Watu wengi ukiwapa kazi unakuwa na wasiwasi hata kulala utashindwa. Kwa …
Usiwape Watu Kiki Kirahisi
Hizi ndiyo zama ambazo watu wanaishi kwa drama sana. Watu wanaishi kwa kutafuta kiki ili maisha yao yaweze kwenda. Usiwashangae watu kufanya mambo ya kijinga, jua wanafanya hivyo kwa sababu ni kazi yao kufanya hivyo ya kutafuta kiki. Tunajua watu ambao wanatafuta kiki ni wasanii tu, lakini kwa sasa hata watu ambao siyo wasanii nao …