Hii Ndiyo Lakini Unayopaswa Kuiondoa Kwenye Maisha Yako Ili Uweze Kufanikiwa

Heri ya mwezi julai rafiki yangu, endelea kupambana kuhakikisha unapata kile unachotaka. Tumekuwa ni watu wa kujiwekea vikwazo sisi wenyewe. Mara nyingine tunajiambia haiwezekani bila ya kujaribu au kuuliza kwa wengine walioweza kufanya. Tumekuwa na lakini nyingi ambazo zimekuwa kama vikwazo kwetu kuweza kufika kule tunakotaka kufika. Ziko lakini nyingi na hii ndiyo mifano elekezi …

Hii Ndiyo faida Ya Kuelewa Kila Kitu

Watu wengi huwa wanapambana kutafuta amani nje yao lakini siku zote amani huwa inapatikana ndani ya watu na siyo nje ya watu. Amani inapatikana ndani ya watu, kama unataka amani katika familia yako, kaa vizuri na wanafamilia wako na yawekeni mambo sawa.  Kama huelewani na jirani yako huwezi kupata amani nje ya yule mtesi wako, …

Kinachofanya Ndoa Nyingi Zisiwe Na Furaha Ni Hiki Hapa

Mpendwa  rafiki yangu, Tuko wote leo hii duniani ni kwa sababu ya matunda ya ndoa. Ni mpango wa Mungu kila mmoja wetu kuzaliwa katika familia. Ndoa ndiyo taasisi ya kwanza duniani, kupitia ndoa ndiyo sehemu ambayo miito yote huzaliwa. Wanandoa wengi wanaishi maisha ya hofu, kila mmoja anamwoga mwenzake na watu wakishaanza kuogopana kila mtu …

Sehemu Pekee Ambayo Hutakiwi Kuwaamini Watu Haraka

Mpendwa rafiki yangu, Hongera sana kwa hatua nzuri unazoendelea kuzipata katika maisha yako. usiache kuwa mtu wa kushukuru hata kama mambo hayaenda kama ulivyopanga, kumbuka kila jambo linatokea kwa sababu, kuwa mtu wa shukrani kwani kukosa shukrani ni kukosa fadhila. Kwenye kila baya kuna zuri ndani yake, furahia kila jambo kwenye maisha yako. Uaminifu ni …

Kama Unataka Kuwa Na Bahati Kwenye Kazi au Biashara Unayofanya

Iko njia ambayo itakufanya mwenye bahati lakini pia kuonekana wa tofauti kupitia kile unachofanya. Kila mtu ana bahati katika maisha yake, lakini bahati huwa haiji ukiwa umeweka mikono mifukoni. Bahati ni pale fursa inapokutana na maandalizi. Kumbe basi, hata kama wewe unataka kupata bahati kupitia kile unachofanya fanya vizuri, kuwa bora sana. Fanya tofauti na …

Wekeza Sehemu Hii Muhimu Kabla Ya Kwenda Kuwekeza Kwenye Biashara

Watu wengi kwa sasa wanaingia katika kufanya biashara lakini kati ya biashara nyingi zinazoanzishwa hazichukui hata muda zinakufa. Na ukitaka kuamini hili angalia tu hata maeneo unayoishi utaamini haya ninayokuambia. Wengi wanaingia kwenye biashara ili tu wapate kipato cha ziada kwa sababu ya maisha kuwa magumu. Siyo wengi wanaoingia kwa kupenda bali wanaingia kwa sababu …

Kila Siku Jifunze Kuwa Na Hiki

Mpendwa rafiki yangu, Karibu matatizo mengi yanayosababishwa na watu mengi yanaanzia kwenye midomo yetu. Midomo yetu inachangia kufanya matatizo mengi kuibuka. Hakuna mtu ambaye anaweza kwenda kugombana na mtu ambaye ni bubu eti kwa sababu amemsema vibaya. Huwezi kuangaika na bubu kwa sababu unajua bubu haongei  lakini sisi tunaoongea tunaua watu wengi kwa ndimi zetu. …

Mambo Mawili Yanayopatikana Pale Fedha Inapokuwa Nyingi Kwenye Mzunguko

Mpendwa rafiki yangu, Fedha ni jawabu la mambo yote hilo kila mtu analijua hilo. Kila mmoja wetu anahitaji fedha kila siku ili kuendesha maisha yake. Ukiwa na fedha nyingi zitakuwezesha kupata kile unachotaka kwenye maisha yako. Lakini umasikini hauna faida yoyote kwani haukusaidii kulipa bili. Namshangaa yule mtu anayejivunia sifa ya umasikini na kuona ni …

Ukicheza Namba Hii Lazima Utafanikiwa

Mpendwa rafiki, Katika mchezo wa mpira wa miguu na hata michezo mingine kila mtu ana cheza namba yake uwanjani. Kila mtu anaingia uwanjani huku akijua anakwenda kufanya nini. Kila namba ina majukumu yake uwanjani.  Na ikitokea mtu anacheza namba siyo yake anaacha namba yake lazima italeta madhara. Kwa mfano, golikipa atoke namba moja akacheze nafasi …

Hiki Ndicho Unachopaswa Kumpa Mtu Anayekuamini

Mpendwa rafiki yangu, Hakuna adimu katika dunia ya sasa kama uaminifu. Unaweza kupata vingi kwenye dunia ya sasa lakini  tukija kwenye uaminifu unakuwa ni adimu sana. Uaminifu ni tabia ya mtu, kama mtu ni mwaminifu kwake yeye mwenyewe ni rahisi kuwa mwaminifu kwa watu wengine. ukiona mtu ni mwaminifu kwa nje basi hata kwa ndani …

Design a site like this with WordPress.com
Get started