Watu wengi huwa wanapambana kutafuta amani nje yao lakini siku zote amani huwa inapatikana ndani ya watu na siyo nje ya watu.
Amani inapatikana ndani ya watu, kama unataka amani katika familia yako, kaa vizuri na wanafamilia wako na yawekeni mambo sawa. Kama huelewani na jirani yako huwezi kupata amani nje ya yule mtesi wako, malizana naye kwanza mtesi wako na amani itapatikana.
Leo wabudha wamenitafakarisha sana wanasema hivi; kuelewa kila kitu ni kusamehe kila kitu. Kwanini wanasema hivyo?
Chukulia mfano, unakutana na mtu anakutukana tu bila sababu badala ya wewe kuanza kumrushia makombora ya matusi, unafikiria tu na kuelewa kuwa mtu huyo huenda ni chizi, au unaweza hata usilitafsiri tusi hilo na kuliachia hapo. Hapo utakua umeelewa kila kitu na kusamehe tu.
Falsafa ya ustoa inatuandaa kiakili kila siku asubuhi lazima tujiandae kukabilliana na kila kitu, tunajiandaa kuwa tutakutana na watu wagomvi, wanyang’anyi, wadhulumaji, matapeli nk hivyo ukikutana na mtu njiani labda anataka kukufanyia kitu ambacho ni kinyume na matakwa yako, badala ya kukasirika na kutaka kulipiza kisasi utajiambia tu nilijua nitakutana na watu kama hawa leo hivyo unamsamehe tu na kuendelea na shughuli zako.
SOMA; Ijue Saikolojia Ya Watu Wengi Katika Kufanya Maamuzi Ya Vitu Mbalimbali
Kumbe basi, kuelewa kila kitu ni kusamehe kila kitu. kwa mfano, vijana wengi ambao wako katika hali ya mabadiliko ya kimwili,kiali na kiroho huwa wanakuwa na matatizo mengi. Muda mwingine wanaweza kuwaona wazee au wakubwa wao kama vile wamepitwa na wakati pale wanaporekebishwa kuwa wanakwenda kinyume. Lakini, wewe kama mtu mzima ambaye tayari umeshapitia hali ambayo vijana wanapitia utawaelewa tu na kuwasamehe.
Mambo mengi yanayotokea katika jamii yetu tungekuwa tunayaelewa wala tusingeumia kichwa badala yake tungesamehe kila kitu.
Unaweza kukuta watu wanalalamika kweli kwanini jua ni kali sana au joto ni kali sana au baridi ni kali sana, sasa kwa kuwa wewe ni muelewa unaelewa kuwa katika maisha yetu kuna vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wetu na vile ambavyo viko nje ya uwezo wetu. Sasa kwa kuelewa hilo utagundua kuwa hivyo ni vitu ambavyo viko nje ya uwezo wetu hivyo unawasamehe tu na kuwaacha walalamike badala ya kuumiza kichwa kupambana nao.
Hatua ya kuchukua leo; jaribu kuwaelewa watu na kadiri ya asili na muda mwingine unapowaelewa watu wasamehe kadiri ya uelewa wao.
Kwahiyo, ukitaka mtoto mdogo afanye kama vile unavyofanya wewe ni sawa sawa na kumhukumu samaki kupanda kwenye mti na nyani kuogelea. Kila mtu ana udhaifu na uelewa wake kwenye maeneo yao tofauti hivyo wachukulie kadiri ya uwezo wao wa akili.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl, Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana