Sababu Ya Pili (2)Kwanini Hutakiwi Kukosa Semina Ya Kuanza Mwaka 2022 Kiushindi

Usipange kabisa kukosa kuhudhuria semina ya kuanza mwaka 2022 kiushindi itakayofanyika januari 3 ya mwaka 2022, uzuri wa semina ni kwamba hutakiwi kusafiri bali utabakia hapo hapo ulipo kwa sababu semina itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasapu. Ili usipange kukosa semina hiyo, anza kulipia mapema, gharama ya semina ni elfu 10, Kama bado hujajiunga …

Hakuna Dhambi Mbaya Kama Hii

Watu wengi wamekuwa ni watu wa kutokuwajibika katika kile wanachopaswa kufanya. Ndiyo maana leo nimeamua kukushirikisha kwamba dhambi mbaya kuliko zote ni dhambi ya kutokuwajibika. Usipowajibika tu kwenye kile unachopaswa kufanya lazima utaleta madhara sehemu nyingine. Usipowajibika katika kazi au biashara yako utajikuta unasababisha madhara sehemu nyingine. Kiongozi asipowajibika katika nafasi yake, wale ambao anawaongoza …

Jiambie Hivi Kila Mara

Kwa chochote unachofanya uwe unajikumbusha kwamba lolote linaweza kutokea. Hatuna uhakika wa kesho wala udhibiti wa yale ambayo yako nje ya uwezo wetu. Usipokuwa na namna ya kujikumbusha utajikuta unakuwa na majuto baadae. Ili kuepuka majuto kwenye chochote kile unachofanya, jiambie kuwa, inaweza kuwa mara yako ya mwisho kufanya kitu hicho. Kauli kama hiyo hapo …

Usiruhusu Hali Hii Iingie Kwenye Kile Unachofanya

Ni kawaida kwa binadamu, pale anapokuwa amepata mafanikio kidogo tu, anajisahau na kuona maisha tayari ameshayapatia. Anaanza kuishi kimazoea na kiburi matokeo yake anakuja kuanguka. Usiruhusu hali yoyote ya mazoea au kiburi kwenye kile unachofanya. Kiburi huwa kina tabia ya kukunyang'anya kile ulichonacho. Na mazoea yanaharibu ubora wa kile unachofanya na hilo linaleta anguko kubwa …

Ujumbe Muhimu Wa Leo Kuhusu Mahusiano Yako

Rafiki yangu, Shabaha yangu ya leo ni kutaka kukuambia kuwa furahia kuwaona watu. Kwa nini ?Kwa sababu, tunaishi kwenye zama za ajabu sana. Watu wanaweka umakini wao kwenye teknolojia kuliko kwenye watu halisi. Ni kawaida kwa sasa kuwakuta watu wakiwa pamoja lakini kila mtu akiwa anaangalia simu yake. Tunaipa simu umakini kuliko hata watu halisi. …

Kwanini Msamaha Siyo Kuvumilia Wala Siyo Kusahau

Je, unajua MSAMAHA siyo kusahau?Ikitokea mtu amekukata mkono wako utaweza kumsahau maisha yako yote wakati unaona jeraha alilokuumiza? Karibu sana upate maarifa sahihi juu ya Msamaha, kupitia kitabu cha Kwanini Msamaha (Why Forgiveness)utajifunza kwanini Msamaha siyo kuvumilia au kusahau. Pata nakala yako leo kwa bei ya ofa, kumbuka zimebaki siku 2 kuisha kwa ofa hii …

Hivi Ndivyo Unavyojidanganya Na Kujipa Matumaini Hewa

Katika haya maisha unapaswa kujua kwamba huwezi kupata vyote kwa wakati mmoja. Lazima kuna mahali utapata machache na mengine utakosa. Kwa mfano, kati ya vitu vitatu vifuatavyo chagua viwili utachagua vipi? Kazi, familia na kula bata? Kwenye maisha lazima ujiambie ukweli kwamba mimi niko tayari kukosa mengine lakini kazi, biashara au familia siwezi kukosa. Huwezi …

Ukikutana Na Mtu Mwenye Akili Hii Muulize Swali Hili

Hata uwe vizuri sana kiasi gani, huwezi ukajitegemea kwa kila kitu. Kwa sababu kujitegemea siyo kujitosheleza. Kadiri unavyotaka kufanikiwa ndivyo unavyozidi kuwahitaji watu wengi zaidi. Na kitu kingine ni kwamba, kadiri unavyojifunza zaidi ndiyo unajikuta hujui. Yaani ukiishi katika falsafa ya aliyekuwa baba wa falsafa mwanafalsafa Socrates ambayo inasema hekima pekee aliyonayo ni kwamba hajui …

Kitu Ambacho Watu Wengi Wanakisubiria Kwenye Maisha Yao

Kwenye haya maisha utachelewa kufika kule unakotaka kwenda kama ukisuburia kupewa ruhusa ya kufanya kile unachotaka kufanya. Watu wengi wanakaa huku wakisubiria mtu fulani aje awape ruhusa ya kufanya kile wanachotaka kufanya. Dunia haiko hivyo, ukitaka kupata kile unachotaka, usisubiri kupewa ruhusa, jiruhusu mwenyewe kuingia kwenye kile unachotaka kufanya. Watu wengi waliofanya makubwa hawakusubiri ruhusa …

Jinsi Ya Kuwakera Watu

Kwenye hii dunia tunayoishi huwezi kuishi bila kuwakera watu wengine. Hata kama wewe huna lengo wa kuwakera wao wenyewe watajikera kwa yale unayofanya. Kifupi kwa chochote kile utakachofanya lazima kuna watu utawakera. Je, wewe ungechagua kuwakera watu wa namna gani? Kwa mfano, ukifanya kazi kwa bidii lazima utawakera wale wavivu ambao hawataki kufanya kazi. Ukichagua …

Design a site like this with WordPress.com
Get started