Kama umekuwa na nidhamu ndogo, au huna kabisa nidhamu binafsi ya kujisimamia utakua ni mtu ambaye ni ngumu kusaidika. Mtu ambaye anasubiri kusukumwa kufanya wajibu wake, anakuwa anaweka ugumu wa kusaidika. Mtu ambaye hawezi kufanya kitu mpaka akumbushwe au kusukumwa ndiyo anajituma kufanya kazi ni mtu ambaye ni mzigo na anakuwa mgumu kusaidika. Mtu ambaye …
Anza Mwaka Wako Kiushindi
Jua Vitu Hivi Viwili Kama Unataka Kufanikiwa
Kitu kikubwa ambacho nimejifunza katika maisha ni kwamba, kama huna mwelekeo, mwelekeo wowote utakuchukua.Kama hujasimama kwa lolote, utaanguka kwa lolote. Usipokuwa na misingi yoyote ile, ni rahisi kuyumbishwa. Ila mtu ambaye ana mwelekeo anajua kule anakoelekea na anajua kile anachosimamia. Leo nakusihi ujue vitu hivi viwili kwenye maisha yako. Moja, jua kile unachotaka ni nini …
Continue reading "Jua Vitu Hivi Viwili Kama Unataka Kufanikiwa"
Tunza Siri Za Mtu Huyu
Kama unafanya kazi, biashara au unatoa huduma yoyote ile unatakiwa kuwajali wateja wako. Wateja ni watu muhimu sana kwenye kile unachofanya. Kwa sababu wateja ndiyo wanakuletea fedha kwenye biashara yako. Kwa kuwa wateja ni muhimu unapaswa kutunza siri zao. Mteja anapokuamini na kukuambia mambo yake, tafadhali tunza siri zake. Watu wakikuamini na wewe waaminishe kuwa …
Wekeza Kwa Watu Hawa Muhimu Sana Kwako
Kama ikitokea umekufa leo usiku, mwajiri wako atatangaza nafasi ya kazi mwisho wa mwezi kuziba nafasi yako. Lakini familia yako, wapendwa wako na marafiki zako watakukosa daima.Usiwe bize sana kuishi maisha na kusahau kutengeneza maisha. Hayo ni maneno ya bilionea Elon Musk. Kwa hekima hiyo hapo juu, watu wanakula maisha lakini wanasahau kuwatengenezea watoto wao …
Hiki Ndicho Kinachotokea Pale Mtu Anapoweka Kipaumbele Kwenye Kazi Tu
Jana tulijifunza madhara ya kufanya kazi bila kuwa na mapumziko. Na tuliona ni kwa namna gani mwili wa binadamu unavyohitaji mapumziko. Kwenye maisha lazima uwe na mlinganyo sawa,ukisema unaweka kazi tu mambo mengine yataharibika. Kwa kuweka kipaumbele mbele kikubwa kwenye kazi tu , utayapuuza maeneo mengine ya maisha yako ambayo yanakuwa dhaifu na kuathiri maisha …
Continue reading "Hiki Ndicho Kinachotokea Pale Mtu Anapoweka Kipaumbele Kwenye Kazi Tu"
Kitu Ambacho Kimepuuzwa Na Watu Wengi Zama Hizi
Katika zama tunazoishi, watu hawapumziki wala hawafanyi kazi. Hapa ninamaanisha kwamba wakati wa kazi mtu anafikiria mapumziko na wakati wa mapumziko mtu anafikiria kazi. Mtu akiwa anakula, uwepo wake hauko kwenye kula bali anafikiria kumaliza aende kufanya kitu kingine. Hii inawafanya hata watu wakila hawaoni ile ladha ya chakula kwa sababu wakati wa kula akili …
Continue reading "Kitu Ambacho Kimepuuzwa Na Watu Wengi Zama Hizi"
Jenga Kitu Hiki Muhimu Kama Una Miliki Biashara
Biashara siyo kununua vitu kwa bei ya jumla na kuviweka kwenye eneo lako la biashara na kuuza kwa reja reja. Kufanikiwa kwenye biashara siyo kazi rahisi kama ingekuwa rahisi basi kila mfanyabiashara angekuwa mbali sana. Wengi tunawaona wanaanza biashara lakini zinakuja kuwashinda. Wewe kama mmiliki wa biashara majukumu yako siyo kuuza na kununua pekee, siyo …
Continue reading "Jenga Kitu Hiki Muhimu Kama Una Miliki Biashara"
Mapinduzi Huwa Hayaletwi Kwa Kukumbatia Kilichopo
Ukienda sehemu yoyote ile kuna mazoea ambayo tayari yameshajengeka kwenye eneo hilo na wanayachukulia kama ukweli na kiwango chao ambacho kila mtu anapimwa nacho. Ukienda wewe na ukafanya kwa utofauti utaletewa upinzani na kuonekana kama ni adui unafanya vitu ambavyo uliowakuta walikuwa hawafanyi. Utaweza kuulizwa hata yale unayofanya, unayafanya kwa mamlaka au amri ya nani? …
Continue reading "Mapinduzi Huwa Hayaletwi Kwa Kukumbatia Kilichopo"
Njia Moja Makini Ya Kujitofautisha Na Wengine
Waswahili wanasema kifo cha wengi ni harusi. Watu huwa wanajisikia vizuri sana pale wanapokuwa wanafanya kitu ndani ya kundi, tena watu wakiwa wengi hujiona wako sahihi hata kama kitu siyo sahihi. Usijifiche kwenye kundi, kwa kuishi kimazoea na kufuata mkumbo. Unatakiwa kuwa wewe kama wewe kwa kuishi upekee wako. Kufanya kile ambacho wengine wanafanya kimewafanya …
Continue reading "Njia Moja Makini Ya Kujitofautisha Na Wengine"