Leo Hakuna Taarifa Ya Habari

Pata picha umejiandaa kusikiliza au kuangalia taarifa ya habari ukiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua dunia inaendaje au nini kimetokea, halafu anakuja mtangazaji wa taarifa ya habari anakuambia zima TV au radio yako nenda kalale leo hakuna habari, je utajisikiaje?Watu wanapenda habari na hata ukiwaambia hakuna habari hawawezi kukuelewa. Na hata habari nyingi unazozisikia …

Utakuja Kumwitaji Tena Baadaye

Milima huwa haikutani ila binadamu tunakutana, wahenga walisema hivyo. Jamii yetu imekuwa na mtazamo wa hovyo na wa tofauti sana. Mtu anapokuwa anahusiana na mtu mambo yanakuwa mazuri lakini wakishindwa kuelewana kwenye kitu kidogo tu, basi kisirani kinaanzia hapo. Sina uhakika kama itakufaa lakini kama umeachana na msaidizi wako kwenye biashara, nyumbani, mpenzi au mchumba …

Hakuna Unachojenga

Biashara yoyote ambayo haina mfumo ni sawa na kujenga nyumba bila msingi, itaanguka muda wowote ule. Mahusiano bila misingi inayoendesha mahusiano hayo ni rahisi kuanguka.Kazi yoyote isiyokuwa na misingi huwa ni rahisi kupoteza mwelekeo. Kitu chochote kile ambacho hakina mwelekeo, huwa mwelekeo wowote ule unauchukua. Kuwa na mfumo wa kuendesha kila kitu kwenye maisha yako. …

Namba Hazidanganyi

Ukiwauliza maswali watu kwamba wanaendeleaje? Watakujibu wanaendeleaje vizuri tu, wengine watasema Mungu anasaidia kwa kweli. Ukija katika upande wa namba majibu wanayotoa watu na namba haziendani kabisa kwa mfano, kwenye biashara, muulize mtu biashara yako inaendaje? Atakujibu inaendelea vizuri tu, Sasa ukitaka kumuuliza namba kwa mfano,mauzo yako yakoje?una wateja wangapi, wangapi ni wapya na wangapi …

Kama Unauchukia Umasikini Huwezi Kuwa Hivi

Umasikini siyo utakatifu wala utajiri siyo dhambi. Kama umasikini unakuumiza na unapenda kweli kubadilika kwenye maisha yako, huwezi kuwa na mjadala kwenye kazi. Kama unataka kufika mbali, huwezi kuwa na mjadala kwenye mambo yako muhimu kama vile uamke asubuhi na mapema ukafanye kazi au ulale. Huwezi kuwa na mjadala kwenye mambo muhimu, yaani ukipanga umepanga, …

Watu Wanakuchukuliaje?

Ni rahisi sana, watu wanakuchukulia kwa namna unavyojichukulia wewe. Ukijichukulia mwaminifu na watu watakuchukulia mwaminifu. Na mara nyingi binadamu huwa tunatoa kile ambacho tunacho. Hatuwezi kutoa kile ambacho hatuna. Hata kama kuna mtu anaigiza hali fulani kwenye maisha hawezi kudumu naye hata siku moja. Watu wanakuchukulia jinsi unavyojichukulia wewe mwenyewe. Tuwe makini, sisi ni kioo, …

Penye Nia Pana Njia

Ukiwa unataka kufanikiwa kitu, utafanikiwa kama kweli umejitoa na kuwa king'ang'anizi bila kujali ukinzani wowote ule. Fuata nia yako ya ndani na hakuna kitakachokuzuia. Dunia itakupisha kama kweli na wewe umejitoa. Hujawahi kuona unawaza kitu fulani halafu unashangaa unakutanishwa na mazingira ya kitu hicho? Au unamfikiria mtu halafu unashangaa anakupigia simu au anakutembelea. Ndani yetu …

Kauli Unayopaswa Kujiambia Pale Unapokutana Na Changamoto

Kwenye maisha mara nyingi vitu vingi huwa hatuvipati kwa urahisi. Huwa tunavipata kwa ung'ang'anizi mkubwa. Hakuna mtu ambaye anaweza kukupa ushindi kirahisi, asili huwa ina tabia ya kumpima mtu ili kuona amejitoaje kwenye kile anachofanya. Ukikutana na ukinzani wowote ule kwenye maisha yako, unapaswa kujiambia,Nina ung'ang'anizi mkubwa kuliko ukinzani wako. Mtu anakupa ukinzani wowote ule, …

Usiongeze Chumvi

Kwenye mchakato wa mauzo , unaweza ukasema ni bora uongeze chumvi kidogo ili uweze kumnasa mteja.Kuongeza chumvi yaani kusema maelezo ambayo hata hayapo ni njia rahisi kabisa ya kumfukuza mteja kirahisi. Ongea ukweli, hata kama upande wa pili hawajui wewe ukishajua nao watakuja kujua. Kuongeza chumvi, kutakupotezea wateja wako wote na mtu akigundua kwamba uliongeza …

Jinsi Ya Kukabiliana Na Mteja Mjuaji

Kwenye mchezo wa mauzo huwa tunakutana na wateja wengi, kazi yako kubwa kama mtu wa mauzo ni kuweza kukamilisha mauzo. Haijalishi umepiga chenga nyingi kiasi gani kama hujakamilisha mauzo unakua huna ulichofanya. Kwa nini tunasisitiza zaidi mauzo kwa sababu mauzo ndiyo moyo wa na fedha ndiyo damu ya biashara. Kama mtu hana moyo wala damu …

Design a site like this with WordPress.com
Get started