Unapoianza siku yako unakutana na mengi, usipokuwa na orodha ya kufanya mambo yako yaani to do list ni rahisi kuhangaika na yale ambayo hata hukuyapangilia. Mambo ambayo hatujayaandika kuyafanya ndiyo mambo ambayo huwa yanatuondolea fokasi kubwa kwenye siku yetu. Unajikuta unatumia muda mwingi kwenye drama ambazo hazina maana kwako.Unatakiwa kuwa na mfumo wa kusema HAPANA …
Mtu Mwenye Maono Makubwa
Jana kuna kauli moja ambayo niliisikia kutoka katika mijadala ya watu, walikuwa wanaongea mengi ila kuna sentensi moja ilinitafakarisha sana. Kauli hiyo ni mtu mwenye maono makubwa huwa hali hovyo. Nikaitafakari na kuona ni kweli, huwezi kumkuta mtu mwenye maono makubwa amekaa vijiweni anakula na vyakula vya hovyo. Kwa sababu, kupitia chakula hata watu ambao …
Hakuna Mafanikio Bila Mateso
Kama kuna mtu anakuambia kwamba unaweza kufanikiwa kwenye jambo lolote lile bila mateso huyo anakudanganya. Pata picha kwa yale mafanikio ambayo unayo, ni mafanikio gani ambayo umeyapata kirahisi bila mateso? Njia ya mafanikio yoyote ile ni ngumu, ina mateso ndiyo maana wengi WANASHINDWA na kuishia njiani. Hakuna mafanikio utakayopata kwa njia ya imani tu, imani …
Njia Ya Kwenda Motoni Imepambwa Kwa Nia Njema
Vitu vingi vinavyoharibu hata afya na maisha yetu ni vile vitu vitamu, angalia sukari ni nzuri lakini ukiizidisha inavyokuletea shida. Kuishi bila mazoezi ni raha kwa sababu huusumbui mwili lakini matokeo yake yanakuja kukuumiza baadaye. Mtu anakuwa anaiba kwa nia njema kabisa, kwa mfano umemwajiri mtu siku akajisikia kuchukua elfu tano halafu ukimlipa mshahara atakuja …
Continue reading "Njia Ya Kwenda Motoni Imepambwa Kwa Nia Njema"
Kinachowezekana Kufanyika, Kifanyike Sasa
Huwa tunajidanganya sana kwa kuahirisha mambo yetu ambayo tunaweza kufanya sasa hivi lakini tunajiambia baadaye. Sina uhakika kama itakufaa lakini, kile unachoweza kufanya sasa hivi, kifanye mara moja usisubiri baadaye. Pata picha wewe mwenyewe ulivyojikosesha au kujikwamisha mambo mengi kwa kujiambia kesho, baadaye au mwakani. Unajionea wewe mwenyewe jinsi ulivyoshindwa kwa kujiwekea vitu mbele?Kama kitu …
Continue reading "Kinachowezekana Kufanyika, Kifanyike Sasa"
Unataka Nikusaidie Nini?
Ni moja ya swali ambalo Yesu alimuuliza kipofu, kipofu akamjibu, nataka kuona tena. Katika maisha ya kila siku hatuwezi kupewa kama tusiposema tunataka nini? Ili ufanikiwe kwenye kitu chochote kile, lazima kwanza ujue unataka nini, kama hujui unataka nini hakuna atakayeweza kukusaidia. Mungu aliyekuumba pasipo wewe kupenda, hawezi kukubadilisha pasipo wewe kupenda. Je, kuna kitu …
Kama Mapigo Ya Moyo Yanafanya Kazi
Daktari yeyote yule, anayekutana na mgonjwa ambaye mapigo yake ya moyo yanafanya kazi, atajituma kwa kila namna kuweza kumsaidia mgonjwa kupambania uhai wake.Lakini, ni ngumu daktari kupambana au kuhangaika na mteja ambaye mapigo yake ya moyo hayafanyi kazi yaani amekufa kwa sababu unakuwa huna la kufanya kwa mtu ambaye amekufa. Hii ina maana gani kwetu? …
Mahusiano Mazuri Ni Maisha Mazuri
Iko hivi rafiki yangu, Mahusiano mazuri ni maisha mazuri na mahusiano mabaya ni maisha mabaya. Hakuna mafanikio yanayopatikana katika mahusiano mabaya, ukitaka kuwa na mafanikio unapaswa kuwa na mahusiano mazuri na wale unaojijusisha nao.Mahusiano mabaya yanaumiza, yanakufanya ushindwe kufokasi katika kazi. Muda mwingi utautumia katika kusuluhisha migogoro badala ya kufanya kazi. Weka juhudi kwenye kujenga …
Huwa Inatokea Lakini Usifanye Kila Siku
Huwezi ukapanga mambo yako na yakaenda vizuri kila wakati. Kuna wakati mambo yanaenda vizuri na kuna wakati mambo yanaenda ndivyo sivyo. Kuna wakati unaanguka kama binadamu lakini katika msimamo wako ulioamua kufanya usiuvunje mara pili. Dharura huwa zinatokea lakini usikubali iwe kila siku kwa mfano, kuchelewa kufika eneo la kazi, biashara au miadi yoyote ile. …
Ung’ang’anizi Wa Muda Mrefu
Watu wengi wamekuwa hawana subira kwenye maisha yao. Wanaanzisha kitu leo na wakiona hakina matokeo ndani ya muda mfupi wanaamua kuachana nacho.Kitu chochote ukitaka kujua kama kitakunufaisha au la unatakiwa ukifanyanye ndani ya miaka 10. Ndiyo, jitoe ndani ya miaka 10 kupitia kile ulichoamua kukifanya na utaona matokeo. Kazi uliyoamua kuifanya jipime ndani ya miaka …