Yuko mtu ambaye anakujua vizuri kuliko hata watu wengine na mtu huyo siyo mwingine bali ni wewe mwenyewe. Utaweza kuwadanganya watu wote lakini ukweli ni kwamba huwezi kujidanganya wewe mwenyewe. Ukiangalia maisha yako, jinsi unavyoishi ndiyo utajua kama unawadanganya watu au la. Je hayo ndiyo maisha yako halisi? Kama siyo kwanini unaendelea kuishi maisha ambayo …
Category Archives: Uncategorized
Hii Ndiyo Hatua Ya Mtu Anayetaka Kufanya Kitu
Siku zote mtu anayetaka kufanya kitu huwa anakua hana sababu za kutaka kufanya bali;Anafanya tu. Kwa mfano, mtu anayetishia anataka kujinyonga huyo basi hataki kujinyonga bali anatishia tu ili aweze kupata kile anachotaka. Watu wengi huwa wanawatishia wale watu wao wa karibu kuwa wanataka kufanya kitu fulani basi wale wa karibu wanawaomba wasifanye hivyo halafu …
Continue reading “Hii Ndiyo Hatua Ya Mtu Anayetaka Kufanya Kitu”
Bado Hujaamua Kukipata Kitu Hiki Ndiyo Maana Hukipati
Mtu mmoja alikuwa anasoma gazeti nyumbani kwake, mara akatokea mgeni akamuuliza vipi mbona mbwa wako analia hivyo? Akamjibu, amekalia msumari, yule mgeni akamwambia kwanini sasa usimtoe?Akamjibu, kama ingekuwa msumari umemchoma vizuri angetoka hapo alipo asingeendelea kulia. Hii ni hadithi fupi, lakini ina funzo ndani yake. Hii iko hata katika maisha yetu ya kawaida wako watu …
Continue reading “Bado Hujaamua Kukipata Kitu Hiki Ndiyo Maana Hukipati”
Jinsi Ya Kuwa Na Nguvu Ya Akili
Utakua mkali sana pale mtu anapokuja kuuchezea au kuushika mwili wako bila ridhaa yako. Je utakua tayari kuuanika mwili wako na watu wauchezee vile wanavyotaka? Kama huwezi kufanya hivyo, kwanini sasa unaruhusu watu waichezee akili yako vile wanavyotaka? Umekuwa ni mteja wa kila habari, huchagui wala kuchuja kile kinachoingia akili kwako. Akili yako ndiyo kiwanda …
Haya Ndiyo Mafanikio Unayopaswa Kuwa Nayo
Iko wazi kila mtu ana ndoto yake hapa duniani. Lakini cha kuchangaza wako watu ambao wala hawana ndoto. Kuna binadamu wengine wako kama vile wanyama wanachojua wao ni kula tu. Wako ambao wanaishi ili wale na wako ambao wanakula ili waishi. Vipi ile ndoto yako uliyokuwa nayo kwa sasa umefikia wapi? Nasikitika kuwa ndoto za …
Continue reading “Haya Ndiyo Mafanikio Unayopaswa Kuwa Nayo”
Fikiria Vitu Vingi Lakini Fanya Hiki Tu
Hakuna mtu anayekatazwa kufikiri, kwanza kitu ambacho mtu hawezi kukuzuia kwa namna yoyote ile aidha wakufunge au wakufanye nini bado unayo nafasi ya kufikiri vile unavyotaka. Na kufikiri ndiyo kazi ambayo binadamu wengi wanaiogopa.Ni kawaida kufikiria mambo mengi sana mpaka inafikia kipindi unashindwa lipi la kufanya unaona yote ni muhimu baada ya kufikiri. Wakati mwingine …
Jinsi Ya Kuilinda Familia Na Jamii Yako Dhidi Ya Hali Inayoendelea Duniani Kwa Sasa
Ukitaka watu wanaokuzunguka wawe makini unapaswa wewe kuanza kuwa makini. Vivyo hivyo kwa vitu vingine. Ukitaka kuilind jamii yako anza kujilinda kwanza wewe mwenyewe. Dunia kwa sasa iko katika vita dhidi ya korona ili uweze kuilinda familia yako anza kujilinda kwanza wewe mwenyewe. Kuwa makini na sehemu unazokwenda kwa kuhakikisha unafuata taratibu elekezi za ugonjwa …
Kabla Hujafanya Chochote Zingatia Hiki
Ili tupate matokeo mazuri kwenye chochote kile tunachofanya lazima kwanza tuwe na maandalizi. Angalia kile unachofanya kinahitaji mahitaji gani ya msingi kabla hujaanza kile unachofanya. Kwa mfano, kama wewe ni daktari kabla hujamfanyia mgonjwa upasuaji unatakiwa kuwa na orodha ya vitu vya msingi vya kufanyia upasuaji kabla hujaanza zoezi la upasuaji. Haipendezi umeanza kazi, mara …
Huwezi Kutafuta Amani Kwa Kuepuka Maisha
Tunaishi kwa sababu tuna amani. Unasoma hapa kwa sababu una amani kama ungekuwa kwenye vita usingeweza kupata hata muda wa kujifunza. Kwa sasa watu wanakosa uhuru wa kufanya biashara, kazi na hata uhuru wa kuabudu kwa sababu hakuna amani. Hofu ya ugonjwa wa Corona imechukua nafasi ya amani. Tusipokuwa na amani ndani yetu hatuwezi kuifanya …
Jinsi Ya Kuepuka Kifo, Maafa Na Hatari Nyingine
Yako mambo mengi katika maisha yetu ambayo tunaweza kuyaepuka kwa kuwa tu waangalifu.Mwandishi mmoja aliwahi kusema, kuishi muda ni kuwa mwangalifu maana usipokuwa mwangalifu utaiacha dunia mapema. Wako watu wengi wanatapeliwa kwa sababu ya kukosa kuwa waangalifu. Kukosa uangalifu katika maisha yako ni rahisi sana kukaribisha kifo, maafa na hatari nyingine. Angalia hasara nyingi wanazopata …
Continue reading “Jinsi Ya Kuepuka Kifo, Maafa Na Hatari Nyingine”