Hakuna mtu anayekatazwa kufikiri, kwanza kitu ambacho mtu hawezi kukuzuia kwa namna yoyote ile aidha wakufunge au wakufanye nini bado unayo nafasi ya kufikiri vile unavyotaka.
Na kufikiri ndiyo kazi ambayo binadamu wengi wanaiogopa.
Ni kawaida kufikiria mambo mengi sana mpaka inafikia kipindi unashindwa lipi la kufanya unaona yote ni muhimu baada ya kufikiri.
Wakati mwingine kufikiri sana, bila kufanyia kazi kile ulichofikiri inakuwa kama vile mtu aliyebanwa na haja yoyote ile akili yake haiwezi kutulia mpaka atimize haja yake.
Methali ya kireno inasema hivi, fikiria vitu vingi lakini fanya kimoja tu.
Unapokosea ni pale ambapo una mambo mengi halafu unataka kuyafanya yote kwa pamoja.
Usipokubali kufanya kitu kimoja kwanza utajikuta unapoteza yote kwa pamoja. Hata waswahili wanasema mshika mawili moja humponyoka hivyo zingatia hili.
Hata kama unayo mengi ya kufanya, huwezi kuyamaliza yote kama hautakua tayari kuanza na kimoja.
Hatua ya kuchukua leo; Haijalishi una fikiria vitu vingi kiasi gani, fanya kimoja kwanza ndiyo mpango mzuri.
Kwahiyo, hata safari yoyote ile inaanza na hatua moja. Ukitaka kufanya hayo yote uliyonayo kichwani anza na kimoja utapata nguvu ya kufanya mengine.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl, Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz
Asante Sana