Mpendwa rafiki yangu,
Huenda kuna watu tokea wazaliwe hawajawahi kuishi maisha yao. Kuishi maisha yako ni kuishi vile upendavyo wewe na sasa hiyo imekuwa ni changamoto ya watu wengi. Kuna gharama za kuishi maisha yako, hivyo kama unataka kuishi maisha ukubali kuzilipa mapema.
Maisha bora ya kuishi maisha yako iwe ni kwenye kazi, biashara na nk ni haya;
Sema kile unachotaka kusema,
Sema kile unachotaka kusema ambacho unajua ni sahihi kwako,fanya tena kile ambacho unataka kufanya ambacho unaamini ni sahihi kwako.
Huwezi kumfurahisha kila mtu ila unaweza kujifurahisha wewe mwenyewe tu hapa duniani na unaweza kujifurahisha vile utakavyo.
Watu wengi wanashindwa kusimama imara katika maisha yao. Hawajiamini katika kile wanachotaka kufanya na kil wanachokijua na hiki ndiyo hupelekea watu wengi kushindwa kuishi maisha yao.
Unapotaka kuishi maisha yako ishi vile utakavavyo na siyo watakavyo watu. Unatakiwa kusimama kwa miguu yako mwenyewe. ukiwategemea watu lazima watakuangusha katika kutekeleza kile unachotaka kuishi.
SOMA; Vishinde Vitu Hivi Vitatu Na Maisha Yako Yatakuwa Bora Sana
Kuwa na maoni yako hata kama wengine watakupa maoni yao. Kila mmoja wetu anatakiwa kuishi kadiri ya maoni yake mwenyewe na siyo maoni ya watu. Tujifunze kuamua na kuishi maoni yetu na siyo ya watu wengine. Jiamini kwenye unachotaka kusema, kuandika ili mradi tu ni sahihi.
Huwezi kuwa mtu bora na mwenyewe mafanikio kama huyaishi maisha yako kikamilifu na umewapa watu wengine nafasi ya kuamua kile wanachotaka wao na siyo kile unachotaka wewe.
Usiogope rafiki yangu, maisha ni mafupi ukiwa unamhofia kila mtu atasemaje juu yaw ewe, unachotakiwa kufanya ni kuishi vile uwezavyo na usiwasikilize wanasema nini.
Hatua ya kuchukua leo; ishi vile upendavyo wewe na siyo wapendavyo watu. Sema kile unachotaka kusema ambacho unajua ni sahihi kwako. Fanya kile unachotaka kufanya ambacho unakiamini na unaona ni sahihi.
Kwahiyo, kama unaishi maisha yako bila kuvunja sheria huna shida na mtu yeyote. Kuishi maisha yako zingatia kutokwenda kinyume na sheria za mahalia.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana