Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kuwa Na Nguvu Ya Akili

Utakua mkali sana pale mtu anapokuja kuuchezea au kuushika mwili wako bila ridhaa yako.

Je utakua tayari kuuanika mwili wako na watu wauchezee vile wanavyotaka?

Kama huwezi kufanya hivyo, kwanini sasa unaruhusu watu waichezee akili yako vile wanavyotaka? Umekuwa ni mteja wa kila habari, huchagui wala kuchuja kile kinachoingia akili kwako.

Akili yako ndiyo kiwanda kinacholinda na kuzalisha maarifa na thamani yote unayotoa. Hivyo akili yako ikiwa vizuri basi na mwili wako utakua vizuri.

Kama unasitiri mwili wako na akili iko wazi ni sawa na uko uchi. Ifunike akili yako kwa kuijaza maarifa sahihi. Kile kinachoingia akilini ndicho utakachokitoa nje hivyo kuwa makini sana na kile kinachoingia kwenye akili yako.

Sasa ukitaka kuwa na nguvu ya akili iko njia rahisi sana ambayo huwa naitumia na niliyojifunza kwa aliyekuwa mwanafalsafa wa ustoa na mtawala wa Roma Marcus Aurelius anasema hivi;

” una nguvu juu ya akili yako lakini siyo mambo ya nje, tambua hili na utakua na nguvu.”

Vitu vyote huwezi kuvitawala na kuvidhibiti isipokuwa akili yako tu. Hata mwili wako huwezi kuudhibiti, ingekuwa uko ndani ya uwezo wako ungejizuia kuumwa na mengine mengi.

Kitu ambacho ni chako na unao uhuru wa kukitumia bila kunyang’anywa ni akili tu lakini vingine siyo vyako iko siku utanyang’anywa na kuvirudisha kwa wenyewe.

“You have power over your mind – not outside events. Realize this, and you will find strength.”
– Marcus Aurelius

Unakosa nguvu ya akili kwa sababu unapambana na mambo ambayo yako nje ya uwezo wako. Mambo mengi yanayoendelea, matukio nk yako nje ya uwezo wako hivyo ukipambana nayo utajikuta huna nguvu.

Kupambana na mambo ambayo yako nje ya uwezo ni kama vile unataka kupambana na dunia iende kama vile unavyotaka wewe na hapo ndiyo mwanzo wa kushindwa.

Unayo nguvu ya kuitawala akili yako na kufikiri kile unachotaka. Na kutawala mambo ambayo yako ndani ya uwezo wako.

Hatua ya kuchukua leo; Pambana na yale mambo ambayo yako ndani ya uwezo wako tu. Akili yako itakuwa na nguvu na hata na hekima.

Kwahiyo, usitake kuwa kiranja wa dunia, kwa kutaka kuinyoosha dunia iende kama vile unavyotaka wewe.
Pambana na yale yaliyo ndani ya uwezo wako tu wala usijibe shida kwani maisha yenyewe tayari ni magumu na wewe unayafanya kuwa magumu zaidi kwa kuhangaika na yale ambayo yako nje ya uwezo wako.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl, Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz

Asante Sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: