Siku zote mtu anayetaka kufanya kitu huwa anakua hana sababu za kutaka kufanya bali;
Anafanya tu.
Kwa mfano, mtu anayetishia anataka kujinyonga huyo basi hataki kujinyonga bali anatishia tu ili aweze kupata kile anachotaka.
Watu wengi huwa wanawatishia wale watu wao wa karibu kuwa wanataka kufanya kitu fulani basi wale wa karibu wanawaomba wasifanye hivyo halafu wanampa kile alichokuwa anakitaka.
Ijue hii, mtu yeyote anayetaka kufaya kitu huwa anafanya kwa mfano, mtu anayetaka kujiua huwa anajiua wala hatishii mtu lakini mtu ambaye hataki kufanya anatishia kwa maslahi yake ya kupata kile anachotaka.
Mtu aliyeamua kufanya kitu huwa hasemi bali anafanya tu. Katika maisha wale wanao ongea huwa siyo watendaji wazuri.
Mtu anayetaka kuandika kitu anakaa chini na kuanza kuandika lakini mtu anayesema nitakuja kuandika huyo hana uhakika na kile anachotaka.
Watu wanaotaka kufanikiwa kwenye kitu fulani huwa wanajituma sana ili wafikie ndoto yao.
Hatua ya kuchukua leo; kuwa mtu wa kufanya na usiwe mtu wa sababu.
Mtu anayejua kile anachotaka huwa anakua hana sababu bali ni kazi tu.
Hivyo basi, maisha yetu yanadai kazi sana. Mtu anayetaka kweli kile anachotaka huwa anakua hana sababu bali anafanya tu, yule ambaye hataki ndiyo anakua anatishia atafanya lakini anayejua anataka huwa anaingia kwenye vitendo moja kwa moja.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz
Asante Sana